Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi hawapo pichani kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi  wa ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Rais Napenda kutoa maoni yangu kuhusu juhudi za kujenga barabara za juu ili kupunguza foleni,lakini nionavyo mimi binafsi hii haitapunguza msongamano wa magari na tutaendelea kuwa ni nchi ya foleni kubwa.njia rahisi na ambayo inatumika katika nchi zilizoendelea kwa mfano nimeona Amstardam- Holland na sasa Kenya na Uganda wamejenga ring road au by pass,hii ni muhimu sana kwa kuwa barabara yenye njia sita ikianzia Kigamboni mpaka Kongowe ikaenda mpaka Goba mpaka Boko hii itapunguza sana foleni katika jiji hili la Dar Es salaam,wenzetu wanafanya hivi sasa sisi tumekazana na flyover ambazo hazitasaidia kuondoa msongamano. haya ndiyo maoni yangui mheshimiwa.

    ReplyDelete
  2. Watanzania tujitahidi kutumia muda wetu mwingi katika kufanya kazi zenye tija katika nchi yetu lakini zaidi tujitahidi kutumia elimu (maarifa) tulizozipata katika level mbalimbali kwa namna itakayo jenga na si kubomoa, tuache kushabikia mambo yasiyo na msingi kwa sababu hayatatusaidia chochote, tuache kuwa watu wa kusikiliza tu bali tuwe watu wa kutafuta ukweli. Haiingii akilini vita ya dawa za kulevya ikamezwa na 'tuhuma' za vyeti feki na chuki za wazi wazi kwa mtu aliyejitoa kwa ajili ya taifa lake. Mh. Rais, mimi nakuunga mkono kwa 100%, tuaje majungu, tuchape kazi na usichoke kuwakumbusha watanzania maana ndio maisha tuliyokuwa kumezoea kuishi, maisha ya majungu majungu na kusahau kazi ambazo ndio msingi wa maendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...