Na Daudi Manongi-MAELEZO
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuulinda mradi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro,Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam utakaogharimu shilingi bilioni 188 na kukamilika mwaka 2019.
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akitoa hotuba kabla ya kuweka jiwe la msingi la barabara za juu eneo la Ubungo.
 
“Tutasimamia pesa izi kikamilifu ili tujenge barabara izi za juu vyema,nawataka Watanzania kusimamia mradi huu ili ukamilike haraka na hivyo Wizara,Mkandarasi na Msimamizi wa mradi ili ulete ukamilike na kuleta tija kwa wananchi hawa”,Aliongeza Rais Magufuli.
 
Amesema katika ujenzi wa mradi huo bilioni 1.9 inatoka Serikalini na bilioni 186 inatoka Benki ya Dunia na ivyo ni muhimu kuulinda kwani ni pesa za Watanzania walipa kodi.
 
Aidha amesisitiza kuwa nchi ya yetu imepata mkopo huu  kwa sababu tunaaminika katika kukopesheka na tunarudisha kwa wakati,amemuomba rais wa benki ya Dunia  kuendelea kuikopesha Tanzania katika miradi mingine.
 
Rais Magufuli ameeleza kuwa mkopo huu kutoka benki ya Dunia una riba ya asilimia 0.5 na unalipwa ndani ya miaka 40 ivyo ni vyema kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...