Na Bashir Yakub.
Yawezekana katika shughuli zako za kila siku unaingia makubaliano mbalimbali kama kuuza na kununa magari, viwanja na nyumba, kutoa huduma, kuajiri na kuajiriwa, makubaliano ya vibarua, makubaliano ya kuagiza mizigo na kupokea mizigo, makubaliano ya kufanya kazi na kulipwa au kulipwa baadae n.k. Makubaliano yote hayo yaweza kuwa kwa maandishi au kwa mdomo.
Vyovyote itakavyokuwa swali la kujiuliza ni kama makubaliano hayo kwa maandishi au kwa mdomo unaweza kuyaita mkataba. Na kama yataitwa mkataba je yanakubalika kisheria. Na je sheria inaweza kukulinda iwapo limetokea tatizo lolote ?.
Tutahitaji pia kujua ikiwa umedhulumiwa katika makubaliano yawe ya maandishi au ya mdomo kama inawezekana kuchukua hatua. Na je ikiwa makubaliano hayo sio mkataba ni ipi hadhi yake kisheria na yataitwaje.
1.AINA ZA MAKUBALIANO.
Kuna aina kuu mbili za makubaliano ambayo yakikidhi vigezo yataitwa mkataba. Kwanza makubaliano kwa mdomo na pili makubaliano kwa maandishi.
( a ) Makubaliano kwa mdomo ni pale unapokubaliana na mtu katika jambo fulani kwa kuzungumza tu. Masharti, vigezo na namna ya utekelezaji wake hufanyika kwa kuzungumza tu.
Mpaka makubaliano yanakamilika hakuna popote yanapokuwa yameandikwa. Jambo la msingi hapa ni kuwa aina hii ya makubaliano inakubalika kabisa kisheria . Ukweli kuwa hayakuandikwa popote katu hauyabatilishi.
( b ) Makubaliano ya maandishi haya ni ya kuandika. Kila mlichokubaliana kinawekwa katika maandishi na wahusika wanasaini. Makubaliano haya nayo yanakubalika kisheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...