Na Hassan Matimbwa

Marehemu TX Moshi alifariki tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya JUMATANO majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo makaburi ya Keko machungwa.

Tarehe na siku ya kifo chake vimejirudia mwaka huu na siku hiyo hua kuna Show ya Msondo ktk ukumbi wa Sugar Ray kwa Sokota. Marehemu TX alijiunga Msondo mwaka 1982 akitokea Polisi Jazz. Miongoni mwa nyimbo alizotunga mara baada ya kujiunga ni pamoja na Ajuza, Asha Mwanaseif, (aliomtungia mkewe), na Ashibaye.
Alitunga nyimbo nyingi lakini nyimbo zilizotia fora sana ni pamoja na Kilio cha Mtu Mzima, Ndoa Ndoano, Piga Ua Talaka Utatoa, Ndoa ya Isihaka Kibene, Kaza Moyo na Ajali.
Wimbo wa Ajali aliutunga baada ya kupata ajali ya kuparamia mti wa mvinje pale Mivinjeni Desemba 16, 2005 iliyompelekea kuvunjika mguu.

Moshi alikua chakaramu na mbunifu wa kutunga vionjo ikiwemo mtindo ujulikanao kama Mambo Hadharani na katika nyimbo alipenda kuchombeza vionjo vyenye kutoa raha na kunogesha wimbo mfano utasikia "we nani", " kidogo tu..kidogo tu", "kwanini lakini", " watoto wanachezea umeme", "dispilin", " fair play" nk.
Wakati wa uhai wake alipitia katika bendi mbalimbali za muziki ambazo ni pamoja na Safari Trippers, Juwata Jazz. UDA Jazz, na Polisi Jazz, ambayo alitokea wakati anajiunga msondo. Tz pis alijaliwa kupata tuzo mbalimbali mfululizo za muziki kama Kilimanjaro Music Award.
Marehemu Moshi alibatizwa jina la TX, na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi aliyekuwa mtangazaji wa Radio Tanzania, marehemu Julius Nyaisanga. Nyaisanga alimbatiza jina hilo kutokana na tunzi zake za uhakika. Nyaisanga alikua mtangazaji wa RTD na kisha vituo vya IPP Media. Jina halisi la TX ni Shaaban Mhoja Kishiwa ingawa alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la Moshi William TX.
Hakika Tx Moshi, aliyezaliwa mwaka 1958 huko Korogwe, Tanga, ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa Msondo na ulimwengu wa muziki wa Dansi Tanzania. Tarehe 29 wana Msondo tumkumbuke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...