KAMATI ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge ya Bunge la Jamhuri ya Uganda
imetembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa lengo la kujifunza mambo
mbalimbali ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko kwa wanachama wake.
Ujumbe wa watu 6 kutoka nchini Uganda ulifanya ziara ya mafunzo katika Ofisi za
Makao Makuu ya Mfuko jana (28/3/2017) ambapo walipata fursa ya kuona na
kuelezwa mbinu na mafanikio ya Mfuko huo.
Wabunge hao ni pamoja na Amos Lugoloobi (Mb), Muwanga Kivumbi (Mb),
Kaberuka James (Mb), Felix Kaluyigye (Mb), Opolot Isiagi (Mb) na Ofisa wa Ubalozi
wa Uganda nchini Tanzania Doroth Kalema.
Akiukaribisha ujumbe huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama
Anne Makinda alisema kuwa Mfuko unajisikia faraja kubwa kupata ugeni huo ambao
umetambua kazi kubwa inayofanywa na NHIF na kuona umuhimu wa kufika na
kujifunza ama kupata uzoefu wa namna ya utekelezaji wa shughuli hasa za utoaji wa
mafao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko Bw. Bernard Konga alitaja makundi
yanayohudumiwa na Mfuko kuwa ni pamoja na Waajiriwa wa sekta rasmi, Kampuni
binafsi, wanachama binafsi, wajasiliamali, watoto chini ya umri wa miaka 18,
wanafunzi pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini.
“NHIF imefanikiwa kuwa na mtandao mkubwa wa vituo vya kutolea huduma ambapo
kwa sasa ni zaidi ya vituo 6,000 na mafao wanayopata wanachama ni mengi ambayo
kwa kiasi kikubwa yanaondoa usumbufu wote wakati anapopata ugonjwa,” alisema
Bw. Konga.
Kwa upande wa ujumbe huo waliupongeza Mfuko kwa kazi kubwa inayofanya lakini
pia kwa ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi yao wakati wowote
wanapokuwa na nia ya kuja kujifunza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga akitoa
uzoefu wa huduma za Mfuko kwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Uganda ambao
walitembelea kwa lengo la kupata uzoefu. Kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya NHIF, Mama Anne Makinda.
Wabunge wakipata maelezo katika Kituo cha Huduma kwa Wateja cha NHIF.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda akiwa na wageni katika
picha ya pamoja.
Wageni wakiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda baada ya kumaliza ziara
yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...