WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi mosi, 2017 Serikali itapiga marufuku matumizi ya pakiti za plastiki kufungashiwa pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.
“Tumekaa na
wenye viwanda na kukubaliana kuwa wanaotengeneza Pombe waziweke katika ukubwa
unaokubalika. “Sasa hivi viroba vimeenea kila kona hata watoto wa shule za
msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo. Kuanzia
tarehe moja Machi, tutakayemkamata ameshika pombe ya viroba, sisi na yeye.”
Ametoa kauli
hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 16, 2017) wakati akizumgumza na maelfu ya
wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili
ya ziara yake mkoani Manyara.
Amesema agizo
hilo linaenda sambamba na vita dhidi ya dawa za kulevya kwani mji wa Mererani
unaongoza kwa matumizi ya dawa hizo haramu.
“Tutawakamata
wanaosambaza, wanaouza na wanaokula. Hapa Mererani kuna bangi, kuna mirungi,
cocaine na heroine. Mkuu wa Mkoa hapa panahitaji operesheni kupambana na dawa
za kulevya. Piteni kwenye vijiwe na kukagua wale waliolegealegea, kisha
tuwapime,” alisisitiza.
Akifafanua
suala la uwekezaji kwenye eneo la Shambalai kutokana na ujumbe ulioandikwa
kwenye mabango, Waziri Mkuu alisema katika eneo hilo zimetengwa ekari 500 kwa
ajili ya EPZA ili kujenga miundombinu mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...