Kutokana na ongezeko la watumiaji wa huduma ya kifedha wa M-Pesa  unaotolewa na Vodacom Tanzania,Takwimu za TCRA zimeonyesha huduma hiyo inatumiwa na watu zaidi ya milioni 8,kampuni imejizatiti kusajili wateja zaidi katika huduma ya ‘Lipa kwa M-Pesa’ sehemu mbalimbali nchini. 
Akiongea na wakazi wa jiji la Mbeya wakati wa Uzinduzi wa duka jipya na promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba Mkuu wa kanda ya Nyasa Macfadyne Minja,
,amesema kuwa huduma hii ambayo ni salama na inarahisisha maisha ya wananchi wengi hususani wafanyabiashara inazidi kukubalika ambapo kwa mwaka jana lengo la kampuni lilikuwa ni kusajili watumiaji 20,000 lakini wamevuka lengo kwa kusajili watumiaji  40,000 nchini kote.
Alisema wateja waliochangamkia zaidi ni wale wanaofanya biashara mbalimbali zinazohusisha kupokea malipo moja kwa moja baadhi zake zikiwa ni biashara za maduka ya jumla na rejareja,migahawa,vituo vya kuuza mafuta ya magari,maduka ya vifaa vya ujenzi.Alisema kutokana na ubora wa huduma hii biashara za aina mbalimbali zaidi ya 1,000 zimejisajili na zinatumia kurahisisha mihamala ya malipo ya kibiashara.
“Katika mkakati wetu wa kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali huduma hii ya ‘Lipa kwa M-Pesa’ inarahisisha biashara na  kuleta usalama hususani kwa kuwezesha watumiaji kufanya biashara bila kulazimika kutumia fedha taslimu kama ilivyo katika mataifa mengi yaliyoendelea,tunatoa wito kwa wafanyabiashara kujiunga nayo na kuwa wa kisasa na kutoachwa nyuma kiteknolojia”.Alisema Minja
Sitoyo alibainisha faida nyingine za kutumia huduma hii ni kuwezesha mfanyabiashara kutuma fedha zake za mauzo kwenye akaunti yake ya M-Pesa bila kutozwa gharama zozote,kufanya malipo mbalimbali yanayohusiana na biashara bila kutozwa gharama za ziada na  kuweza kutoa fedha kwa mawakala wa huduma ya M-Pesa kwa gharama yenye unafuu mkubwa.

“Ni rahisi sana na nafuu kutumia huduma ya M-Pesa kufanya mihamala ya malipo kwa kuwa haina gharama zozote za ziada zaidi ya  kukatwa thamani ya bei ya bidhaa anayonunua mteja tofauti na kutoa fedha taslimu kwenye akaunti ya M-Pesa ambapo kuna makato ,huduma hii pia haichukui muda kufanya mhamala wa malipo”.Alisema  Minja.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu alisema“Vodacom inao mtandao mkubwa wa wafanyabiashara ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya kurahisisha biashara zao kwa kutumia huduma ya M-Pesa ambao wako tayari kumwelekeza mteja anavyoweza kufaidika kwa kutumia huduma hii hususani kukoa fedha zake za makato ya kuitumia.Hivi sasa tunatoa ofa maalumu kwa watumiaji wa huduma hii ambapo kwa kila mhamala anaofanya mteja anapatiwa muda wa bure wa maongezi ambapo kwa upande wa mfanyabiashara atapatiwa zawadi kati ya shilingi 2,000/- hadi 100,000/-kwa kila mhamala kulingana na thamani ya mhamala unaofanyika kwa kuitumia”Alisema Materu.
 Baadhi ya washindi wa bahati nasibu iliyoendeshwa jana wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba na Uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lilipo katika Jengo la Raphael Group Uyole jijini Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na wakiongozwa, Macfadyne Minja(wanne kushoto) ambaye ni msimamizi Mkuu wa kampuni hiyo kanda ya nyasa.
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Grace Themistocleous (kushoto) akimuhudumia mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika Duka jipya la kampuni hiyo lilifunguliwa jana katika Majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya ,Wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima..

 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wao walifika katika duka jipya kupata huduma mbalimblai katika duka jipya la kampuni hiyo lililozinduliwa jana katika majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya, Wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamefurika nje ya duka jipya la Vodacom Tanzania katika majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya wakati wa Uzinduzi wa duka hilo na kujinunulia simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...