Benny Mwaipaja, WFM, Kyela

UJENZI wa meli mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani Mbeya, MV Njombe na MV Ruvuma, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 na kwamba meli hizo zinatarajiwa kufanyiwa majaribio Ziwa Nyasa, mwishoni mwa mwezi Februari na kukabidhiwa rasmi Serikalini mwezi Machi, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro MarineTransport Ltd ya Jijini Mwanza, inayounda meli hizo, Mhandisi Saleh Songoro, amesema hayo wakati ujumbe wa Serikali ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea Bandari hiyo ukiwa katika zaira ya kukagua hali ya biashara mipakani mkoani Mbeya.

Amesema kuwa kukamilika kwa meli hizo mbili za mizigo za kisasa zenye uwezo wa kubeba tani elfu moja (1,000) za mizigo kila moja na kugharimu shilingi bilioni 11, kutaiwezesha Kampuni hiyo kuanza kuunda meli nyingine ya tatu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo.

Pamoja na meli hizo, Mhandisi Songoro amesema kuwa mradi huo pia umewezesha kujengwa kwa cherezo cha kwanza na cha pekee kitakacho iwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA katika uundaji wa meli na kuzifanyia matengenezo meli nyingine za ndani na nje ya nchi zikiwemo Malawi na Msumbiji.

Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bandari ya Itungi, Bw. Ajuaye Msese, amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuunda meli hizo ulikuwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa vyombo vya baharini vya kusafirisha abiria na mizingo ndani na nje ya nchi kupitia Ziwa Nyasa.
Meli mbili za Mv. Ruvuma na Mv Njembe zikiwa katika cherezo katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, zikiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio ndani ya Ziwa Nyasa Mwishoni mwa Februari, 2017.
Bw. Juma Nassoro akipaka rangi meli ya mizigo ya Mv Ruvuma, ikiwa ni hatua za mwisho wa ukamilishaji wa uundaji wa meli hiyo yenye uwezo wakubeba tani 1000 za mizigo itakayokuwa ikifanya safari zake Ziwa Nyasa, wakati Ujumbe wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ulipofanya ziara katika Bandari ya Itungi, wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, Bw. Ajuaye Msese akitoa maelezo mafupi kuhusu Bandari ya Itungi, na majukumu yake kwa ujumla kwa wageni waliotembelea Bandari hiyo mkoani Mbeya. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mfumo wa kuongoza meli katika chumba cha nahodha wa meli ya Mv Njombe, huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biasha na Uwekezaji Prof Adolf. Mkenda, akiangalia kwa makini mfumo huo wa kisasa namna unavyofanya kazi.
Baadhi ya wajumbe wa Serikali waliofanya ziara katika Bandari ya Itungi mkoani Mbeya kujionea uundwaji wa meli mbili za mizigo wakishuka kwenye ngazi baada ya kumaliza kukagua meli ya Mv Njombe inayotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd inayoshughulika na kutengeneza vyombo vya usafiri vya majini katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...