Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameitaka nchi ya Uingereza kutazama uwezekano wa kufanya biashara na Tanzania kwa kununua bidhaa zilizoongezwa thamani badala ya hali ya sasa ambapo nchi hiyo imekuwa ikinunua bidhaa ghafi ilihali ikiingiza nchini bidhaa zake za viwandani.

Dkt. Mpango ameyasema hayo alipokutana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Biashara Bw. Lord Hollick ailipo tembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam. 

Amesema Tanzania inataka kuona inauza bidhaa zake zenye thamani ambazo zitatokana na maendeleo makubwa ya viwanda hapa nchini ikiwa ni Sera ya nchi kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025. 

Nchi ya Uingereza imekuwa ikifanya biashara na Tanzania kwa kiasi kikubwa na takwimu zinaonesha nchi hiyo inaingiza bidhaa zenye thamani mara nane ya Tanzania jambo ambalo linatakiwa kurekebishwa ili biashara iwe na manufaa kwa pande zote mbili. 

Miongoni mwa bidhaa ghafi ambazo zimekuwa zikisafirishwa kwenda uingereza ni pamoja na Chai, kahawa na madini ya vito huku Uingereza ikiingiza bidhaa za viwandani zenye thamani kubwa ikijumuisha mashine (mitambo),vifaa vya umeme, bidhaa za plastiki na madawa. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akieleza kuhusu juhudi za Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara wakati wa mkutano na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Mkutano walioongozana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick, wakisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kuhusu umuhimu wa kufanya biashara ya bidhaa zilizoongezwa thamani ili kukuza viwanda vya ndani, wakati wa mkutano huo jijini Dr es salaam.
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Msalato Dodoma, Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kulia) akisisitiza kuhusu kuendelea kuimalisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Uingereza huku Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...