Jumamosi Februari 18,2017,kumefanyika kikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017. 

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mamia ya wachungaji,viongozi na waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro. 

Mnenaji mkuu katika kikao hicho alikuwa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala. 

Akizungumza wakati wa kikao hicho Askofu Dkt. Makala aliwapongeza viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa kanisa hilo,Mchungaji Jakobo Mapambano kwa kuandaa sherehe ya kumuaga Askofu Nkola ambaye amekuwa askofu wa Kanisa hilo tangu tarehe 24.10.1993. 

Askofu Makala alitumia fursa hiyo kuwaonya waumini wa kanisa hilo kutokuwa na tamaa ya madaraka ya uongozi kwa nafasi itakayoachwa na Askofu Nkola hili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza na kusisitiza kuwa ni vyema kiongozi atakayeziba nafasi hiyo apatikane kwa utaratibu unaotakiwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasalimia viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakati akiwasili katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga kuhudhuria kikao chakikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017 .Kulia ni Makamu wa Askofu Dayosisi ya Shinyanga mchungaji Aaron Malyuta
Ndani ya ukumbi wa NSSF: Kushoto ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano,katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala baada ya kuwasili ukumbini.
Maombi yakiendelea baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...