Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wakala uuzaji wa mafuta kwa pamoja, Bw. Michael Mnjinja akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na uuzaji  wa mafuta hapa nchini

Na Yassir Adam, Globu ya Jamii.
WAKALA wa uuzaji wa mafuta  kwa pamoja  na Petroleum Bulk Procurement Agency imedhamiria kuhakikisha bei ya mafuta nchini inashuka kwa kiwango kikubwa hasa baada ya kuanzisha utaratibu mpya wa kuwa na zabuni kwa kila meli inayoleta mafuta nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha utaratibu mpya wa zabuni,  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wakala uuzaji wa mafuta kwa pamoja, Bw. Michael Mnjinja amesema kuwa kwa sasa kila meli itakuwa na zabuni yake na mpaka sasa wameshapata meli sita tofauti kwa mafuta ya dizeli mbili, petrol tatuna mafuta ya ndege pamoja na ya taa meli moja.
Mnjinja amesema kuwa mpaka sasa wameweza kupata premium ya bei ya chini kwa dola 18 na dola 14 ambapo kutokana kwa kushuka kwa bei hiyo kunaleta unafuu katika kupanga bei za mafuta nchini na yatashuka bei tofauti na mwanzo waliweza kupata premium kwa dola 19.

Ameyataka makampuni ya ndani na nje ya nchi kujitokeza kuja kujisajili kwani kwa mwaka huu wameweza kupata kampuni moja tu kutoka nchini ila hawataweza kuruhusu tena makampuni kutoka nje kuwania zabuni za uuzaji wa mafuta, na mabli na hilo zabuni hizo zitakuwa znafanyika kila mwezi.
Baadhi ya wadau wa mafuta wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...