Akiongea na mtandao huu kwa niaba ya Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamni wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bi. Nandi Mwiyombella (pichani), amesema wakiwa kama wadhamini wakuu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara,Wanazitakia kila la kheri timu ya Yanga na Simba katika mzunguko wa kwanza kwa timu hizi kubwa hapa nyumbani zitakazomenyana siku ya jumamosi ya tarehe 1 mwezi Oktoba katika uwanja wa Taifa jijini Da res Salaam. 

"Naamini kwamba mchezo huo utakuwa mzuri na wakuburudisha washabiki wote wa timu hizi watakaofika uwanjani kuushuhudia kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangia msimu huu kuanza.
"Pia napenda kuwatoa wasiwasi wapenzi wa mchezo huu ambao hawatapata na nafasi ya kufika uwanjani kwani Vodacom Tanzania haitawaacha mbali na matokeo yatakayokuwa yakiendelea uwanjani hapo”LIVE” ili kupata matokeo ya mchezo huo ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi cha ‘Soka bando’ na utakuwa unapata frusa ya kupata matokeo kiurahisi kabisa popote pale ulipo ya timu yako uipendayo kati ya Simba na Yanga.
Kifurushi hiki ni chenye gharama nafuu ya shilingi 500/- tu na ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote kwani kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa masaa 24. 
Ili kununua kifurushi hiki unachotakiwa kufanya mteja ni kupiga namba *149 * 01#,  chagua "Ofa mpya" halafu chagua ‘Soka Bando’. Baada ya hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga” “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya Mspoti.vodacom.co.tz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...