Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu wa ufukweni  (Beach Soccer), Ally Bashiru 'Adolph' akizungumza kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Timu ya Taifa ya Ivory Coast unaotarajiwa kuchezwa kesho katika kiwanja cha Karume Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Alfred Lucas na Nahodha wa timu hiyo Ally Rabby (Kushoto).

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya  mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) Ally Sharif 'Adolph' amesema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kuweza kuhakikisha wanapita katika hatua hii ili kuweza kuingia kwenye fainali za mataifa Afrika Desemba.

Akizungumza kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho katika uwanja wa Karume, Adolph amesema wachezaji wote wapo vizuri na wameweza kuonyesha hamasa kuelekea mechi hiyo ambapo kama watafanikiwa kushinda wataingia moja kwa moja kwenye fainali hizo.

Timu hiyo inatarajiwa kukutana na Ivory Coast utakaopigwa majira ya saa kumi alasiri na utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Uganda.

Mwamuzi wa kati anatarajiwa kuwa Shafiq Mugerwa akisaidiwa na Ivan Bayige na Muhammat Senteza. Msimamizi wa muda akiwa Tsalaraza Maolidy kutoka Madagascar na msimamizi wa mechi ni Reverien Ndikuriyo Kutoka nchini Burundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...