Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) imeshiriki katika Mkutano wa kwanza wa TEHAMA ambao umeandaliwa na Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. 
 Katika mkutano wa TEHAMA, TTCL ilipata fursa ya kuonesha huduma na bidhaa mbalimbali ambazo zimechangia katika ukuaji wa matumizi ya TEHAMA nchini na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa. 
 Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) akiwa msimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo Mahiri cha Kutunzia Taarifa(IDC) imefanikisha kuunga Taasisi za Umma na za Binafsi kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa wakati na ubora kwa wananchi.
 Hivi sasa, TTCL inaendelea na utekelezaji wa mradi wa mabadiliko ya kibiashara wenye lengo mahusus wa kuboresha huduma na bidhaa, miundombinu ya mitandao wa mawasiliano ya simu za mezani, mkononi na Data ili kutoa huduma bora, uhakika kwa wateja wake.
 -   Afisa wa TTCL, Diana Obed  akitoa maelezo ya bidhaa ya TTCL 4G  kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura   na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Clarence Ichwekeleza katika Mkutano wa kwanza wa TEHAMA ambao umeandaliwa na Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Mshiriki wa  Mkutano wa TEHAMA akipata maelezo ya huduma ya 4G LTE 
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura akizungumza na mshiriki wa mkutano wa TEHAMA, uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...