Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau wa Michezo aliowaalika ubalozini hapo wakati wa kuiga timu ya Tanzania ya Olimpiki.
Mdau Frank Eyembe akibadilishana mawazo na Kocha wa Kuogelea Sheha Mohammed wakati wa hafla ya kuiga timu ya Taifa ya Olimpiki,iliyoandaliwa na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza
Msosi wa nguvu mezani.
Mh Balozi akikabidhiwa tuzo maalum na mkuu wa msafara Hassan Jarufu iliyotoka katika kamati ya Michezo ya Olimpiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Nyumba ya Balozi lazima itakuwa inakula bili ya gesi kubwa sana hasahasa wakati wa winter.

    Maana nyumba ukuta wa vioo kama vile nyumba zilizopo ktk mitaa ya ufukwe wa bahari Dar-es-Salaam ambapo kuna joto sana.

    Wizara ya Mambo ya Nje iifanyie angalau window double glazing nyumba hii ya makazi rasmi ya balozi wa Tanzania jijini London kupunguza ankra ya bili za kupasha joto jumba hili la makazi ya Balozi.

    Mdau
    Barabara ya Toure Drive Road
    Ufukweni, Dar-es-Salaam.

    ReplyDelete
  2. Mkuu wa msafara alichovaa shingoni ndiyo medali tuliyopata London Olympic 2012?

    Mdau
    Michenzani.

    ReplyDelete
  3. What is it wanamichezo wetu wanatakiwa kufanya ili waweze kushinda michezo ya kimataifa?

    Na sisi wengine tunatakiwa kuwasaidiaje ili waweze kufanikiwa?

    ReplyDelete
  4. hamna haja ya sheree hiyo hao wamepoteza pesa za taifa tu

    ReplyDelete
  5. kwa sherehe tu na kula hatujambo.
    Lakini kufanya vizuri kimichezo na kiuchumi.... tunapiga domo tu.

    ReplyDelete
  6. Au walikuwa wanashangaa mabus na treni? But wenzetu wanajianda more than 3 yrs before ila cc mwezi 1, shame on you angalieni Kenysa na Uganda, their very serious,

    ReplyDelete
  7. Hiyo nyumba ipakeni rangi basi, inaanza kuwa nyeusi wakti rangi inayotakiwa ni nyeupe.

    ReplyDelete
  8. tuunde tume ya uchunguzi ilil tujue chanzo cha kufanya vibaya.... naomba niwe mjumbe angalau niambulie perdiem.....na ole wao wakiniteua...lazima niende London tukachunguze viwanja vya olympic.....inawezekana havijafikia standard ya Bongo.....ndio maana tunashindwa.....

    ReplyDelete
  9. Tatizo la Kamati ya Olimpiki Tanzania ni kutokuwa makini na uchaguzi wa wachezaji. Hawa waliokwenda London ndiyo baadhi ya wale waliokwenda Beijing 2008 na wakatoka mikono mitupu. Lakini bado baada ya miaka minne wanachaguliwa tena kuwakilisha taifa. Je huu siyo ufisadi?

    ReplyDelete
  10. Watanzania, watanzania, watanzania wangu, mtamlaumu nani kwa kuniua pole pole kama hamtaanzia na ninyi wenyewe kila mmoja?
    Tujifunze kukiri uhaba wa juhudi zetu kila mmoja kwanza. Mimi nawapongeza hao waliotuwakilisha na binafsi namsaidia mwanangu kwenye ndoto yake ya kushinda medali Rio 2016. Kila mmoja afanye hivyo kwanza sasa na tujali michezo.
    Hongera waliotuwakilisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...