JENGO la ambalo liko katika hatua za mwisho za ujenzi lililopo katika makutano ya Mtaa wa Samora na Mkwepu jijini Dar limenusurika kuteketea kwa moto jioni ya leo baada ya moja ya Ghorofa katika jengo hilo kushika moto na kuteketeza viyoyozi vilivyokuwepo katika ghorofa hiyo
Mashuhuda wameeleza kuwa moto umeanza majira ya saa 11  kwa kuanza kufuka katika ghorofa ya tatu. Chanzo cha moto hakifahamika mara moja.
Moshi ukitanda angani wakati moto ukiendelea kuwaka katika Jengo lililopo  mtaa wa Mkwepu na Samora jioni ya leo, jijini Dar es Salaam.
Jeshi la zimamoto likiwa katika harakati za kuzima moto katika jengo lililopo Mtaa wa Samora na Mkwepu jijini Dar es Salaam jijini leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...