Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa nje ya jengo la jumba la makumbusho la mkoa wa Iringa akiwa katika mavazi ya Chifu wa Wahehe
Mratibu wa mradi wa Fahari Yetu Bw Jimson Sanga akitoa maelezo kwa Balozi Dr Mahiga kushoto
WAZIRI wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustino Mahiga wa nne kushoto akiwa katika vazi la kichifu wa Kihehe na viongozi mbali mbali baada ya kuzindua jumba la makumbusho la mkoa wa Iringa ,wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na wa watano kutoka kushoto ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Iringa Bi Ritta Kabati akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa MOrogoro Bw
Kebwe Steven Kebwe
Watenda kazi wa Makumbusho hiyo kupitia mradi wa Fahari yetu
Mratibu wa mradi wa Fahari Yetu Bw Jimso Sanga kulia akiagana na balozi Dr Mahiga
Na Matukiodaima Blog
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amepongeza jitihada za chuo kikuu cha Iringa kwa kuwa karibu na serikali ya mkoa wa Iringa katika uanzishwaji wa jumba la makumbusho la mkoa (Iringa Boma) kwa ajili ya kuendeleza kutunza tamaduni za mkoa wa Iringa na kuongeza thamani ya utalii katika mkoa na nyanda za juu kusini.
Asema anaamini chuo kikuu cha Iringa kinatekeleza sera ya Taifa ya ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Balozi Dr Mahiga aliyasema alitoa pongezi hizo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jumba la Makumbusho la mkoa wa Iringa mradi unaoendeshwa na chuo kikuu cha Iringa kupitia mradi wa Fahari Yetu , hafla zilizofanyika kwenye viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa makumbusho hayo ya mkoa wa Iringa yatumike kama chombo cha kuchochea maendeleo kukuza na kutunza tamaduni za mkoa ili kuleta maendele ya nchi yetu kwa kuongeza thamani ya utalii.
Pia alisema suala la uhifadhi na ukuzaji wa utamaduni ni suala linalopewa uzito mkubwa duniani kote hivyo chuo kikuu cha Iringa kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Iringa wamebuni jambo jema ambalo linapaswa kuendelezwa kwa nguvu zote.
“Mataifa mbali mbali anayojitambua hutumia fedha na raslimali nyingi sana kuhakikisha jambo hili linafanikiwa kwa kiwango cha juu ….hivyo basi wananchi wa mkoa wa Iringa mnapaswa kujivunia na kutumia fursa hii ya kupata makumbusho ya mkoa ndani ya jengo hili la kihistoria kuwa mmeletewa nguvu ya kushikilia tamaduni na mila zetu za makabila ya nyanda za juu kusini zisiteteleke”.
Alisema balozi Dr Mahiga kuwa amefurahi sana kuona chuo kikuu cha Iringa kinafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya mkoa kuendelea kuhifadhi tamaduni za wananchi wa nyanda za juu kusini.
“ Chuo chetu kikuu cha Iringa kimekuwa mbele kwa kutoa kipaumbele katika masuala ya kukuza utalii na utamaduni wa mtanzania na hasa kwa kutoa wahitimu katika sekta hii ya utamaduni nchini ….walioandaliwa ili kulisaidia Taifa katika Nyanja hii ya utalii…. Hivyo basi ni wito wangu sasa kwenu kwamba mzidi kuboresha mitaala yenu mkiwa ndio chuo cha kwanza binafsi nchini ili kuujenga zaidi mkoa wa Iringa katika utunzaji wa utamaduni kwa kufanya tafiti zaidi hasa katika eneo la utamaduni na utalii ( Cultural Anthropology and Tourism) ili kuipa jamii na wadau wote uelewa mpana zaidi wa umuhimu wa kutunza na kukuza utamaduni wetu na utalii kwa ujumla kwa maendeleo ya jamii zetu”
Katika hatua nyingine waziri Balozi Dr Mahiga ametumia nafasi hiyo ya uzinduzi wa makumbusho hayo kumshukuru Rais Dr John Magufuli kwa kumteua kuwa mbunge na baadae kumteua kuwa mmoja kati ya mawaziri wake katika baraza lake la mawaziri na kuwa katika uongozi wake kamwe hatamuangusha Rais .
Alisema kabla ya kuteuliwa alikuwa mmoja kati ya wana CCM ambao walijitokeza kuomba kuteuliwa na chama kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge japo kura hazikutosha kutokana na kuishi nje ya mkoa wa Iringa kwa muda mwingi kama balozi japo kurudi kwake serikalini ni heshima ya wana Iringa na Taifa kwa ujumla ambayo Rais Dr Magufuli alimpa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...