Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa. Makame Mbarawa (MB) amezindua rasmi Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) tukio lililofanyika mapema leo Juni 25.2016, Jijini Dar es Salaam.

Akisoma hutuba ya ufunguzi wa Baraza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho kwa niaba ya Waziri Profesa Mbarawa, Amelitaka Baraza hilo kufanya kazi kwa moyo mmoja katika hali ya kuifufua TAZARA kiutendaji na ufanisi kama ilivyokuwa zamani.

Akisoma hutuba hiyo, aliwapongeza viongizi wa wanaounda Mamlaka hiyo akiwemo Mhandisi Bruno Ching’andu kwa kuteuliwa kwake kuongoza Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia na viongozi wengine pamoja na wafanyakazi wote.

Ambapo alisema kuwa, ni dhahiri hatua ya leo imefikiwa baada ya jitihada kubwa na hasa tukitilia maanani hali ya kifedha ambayo TAZARA inapitia katika kipindi hiki. Hivyi kuwapongeza kwa uamuzi huo kwani Mabaraza yana umuhimu mkubwa katika maeneo ya kazi na yameonyesha mafanikio makubwa kila yalipoanzishwa kwani yameweza kuongeza uhusiano mwema kati ya Manejimenti, Vyama vya Wafanyakazi na wafanyakazi kwa upande mwingine.

“Mabaraza haya ni dhana ya ushirikishwaji ikiwa na maana kuwapatia wafanyakazi fursa ya kushauri juu ya masuala ya utendaji kazi, sera za taasisi, ufanisi wa kazi, mazingira ya kazi, ustawi wa wafanyakazi katika elimu, nidhamu, vyeo, pamoja na motisha kwa wafanyakazi. Pia dhana hii ya ushirikishwaji ni kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 kifungu cha 108.

Pia ni kwa mujibu wa Sheria ya majadiliano katika Utumishi wa Umma Na. 19 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Pia Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 kifungu Na. 73 (1 - 3).

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho(wa pili kutoka kulia) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa juu wa wafanyakazi wa TAZARA. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (Katikati) akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Wafanyakazi wa TAZARA. (Picha zote na Andrew ).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...