Na Sultani Kipingo
Habari za uhakika na kusikitisha zimetufikia kuwa mwanaharakati Ras Bupe Bakweresa Karudi, maarufu pia  kama kaka Ras Bupe Mkushi  (pichani kushoto), amefariki dunia katika hosptali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kupata ajali ya gari.
Ras Bupe ameacha mke na watoto. Mke na mtoto wake wa kiume wameshawasili nchini kutokea Uingereza. 
Msiba upo Mbezi Beach mtaa wa Almasi off Ally Sykes Close jijini Dar-es-salaam.
 Marehemu Ras Bupe Bakweresa Karudi alikuja nchini Tanzania katikati mwa miaka ya 70 akifuatana na mkewe na watoto wawili Kiyenda (msichana) na Nyamiche mvulana. Ras Bupe Karudi alikuja kumuomba marehemu baba wa taifa mwalimu Nyerere hili atoe idhini kwa watu weusi wa visiwa vya Karibian vya Jamaica warudi Afrika (Tanzania) kama nyumbani kwani ndio asili yao.
Baada ya kukubaliwa maombi yake, Marehemu Bupe akaungana na wanaharakati wenziwe hapa nchini wakiwemo marehem Prof. Joshua Mkhululi aka Prof. Keneth Edward, Marehem Ras Kwetenge Zanaki Sokoni (Wa Jamaica) pamoja na  wengine ambao wapo hai Imani Mani wakaungana na wenyeji wao Said Jazbo Vuai, Isza Suleiman na Ebrahim Makunja au Kamanda Ras Makunja kiongozi ambapo wakasajili chama cha ushirika chenye jina la UHURU, UMOJA NA MAENDELEO chenye makao kule Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakiwa wanajishughulisha na mipango ya kilimo na kumiliki maroli ya usafirishaji. 
Marehem Kaka Ras Bupe atakumbukwa sana kwa harakati zake zake za kuupigania uafrika na kuwahamasisha raia wenye asili ya kiafrika kurudi Tanzania.
-----------------------------------
Yes, it’s a sad reality but the word going round town that Ras Bupe Mkushi has gone to join the ancestors are true. 
It was last Friday May 20, that he took his last breath, after fighting a tetanus infection. He was the victim of a motor vehicle accident on May Day (May 1st), from which he incurred some leg wounds. His body will be put to rest next Wednesday at  Mbezi Beach in Dar es salaam. This date has been chosen so that family members, from outside of the country can attend the burial. 
- Imani Mani
Ewe Mola mlaze pema mahali peponi marehemu 
Bupe Bwakweresa Karudi 
Amen



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2016

    Kweli mwanaharakati Mungu akupumzishe peponi,tukikukumbuka enzi zenu na mbwiga wako mwenyewe ulipenda kumwita kaka Makunja na mgari wenu katika jiji mnapasua ! kila mtu ulikuwa unaongea na kucheka naye
    Jah Bupe kalale pema peponi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2016

    Mungu amlaze mahala pema peponi Ras Bupe mpiganaji,mwanaharakati uliyeupigania uafrika,tutakukumbuka kwa mengi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2016

    Jah Bupe Karudi huyu mwanaharakati ndiye aliyemuunganisha kamanda makunja kujiunga na wale Umkhonto Usizwe(spear of the Nation)kuchukua wapiganaji wa ANC mazimbu Morogoro baadaye inasemekana mpaka kwa makaburu,jamaa walikuwa wanaharakati si mchezo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2016

    huu msiba mzito Bube atunaye tena kiwili wili hatunaye tena kiroho tupo pamoja naye,enzi zile za miaka ya 80s na yule kamanda Makunja wajamaa walikuwa wamejipanga sana ,cha ajabu yale magari yao yalikuwa na rangi ya kijeshi fulani na bila kusumbuliwa wanapita kila kona

    ReplyDelete
  5. Rest in peace, bro Bupe.

    ReplyDelete
  6. REST IN POWER BREDREN KARUDI. Almight amekupenda zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...