Mwenyekiti wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) Bw. Erick Chrispin akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa hilo unaofanyika kila mwisho wa mwezi jana jijini Dar es Salaam. Mada kuu katika mjadala huo ilikuwa ni “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake”
Afisa Mtendaji Mkuu wa Asasi ya Open Mind Tanzania (OMT) ambaye pia ni Mratibu wa Programu ya Kukuza Ajira zenye staha jijini Dar es Salaam(YEID) Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha maada kuhusu misingi ya ujasiriamali wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
Meneja Matukio na Ushirikiano wa Asasi ya Buni Innovation Hub Bi. Maryam Mgonja akielezea kuhusu namna asasi yao inavyofanya kazi wakati wa mjadala kuhusu “Jinsi gani Asasi zinawezakutumia Ujasiriamali wa Kijamii katika kuibua na kuhakikisha inafikia malengo yake” jana jijini Dar es Salaam. Mjadala huo uliratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
Pamoja na kupongeza jitihada za kupunguza umasikini nchini (sio kumaliza umasikini - umasikini hautaisha duniani popote pale), je, hatuwatengi wengi wasiojua Kiingereza au hayo yanayooekana kwenye hayo mabango hutafsiriwa kwa Kiswahili?
ReplyDeleteTunaweza kuwa tunapunguza umasikini na tunaua polepole Kiswahili!