​Mstahiki Meya wa Manipsaa ya Iringa, Mh. Alex Kimbe na Mkuu wa Wilaya ya Iring, Mh. Richard Kasesela, Aprili 30, 2015 waliungana na walimbwende walio shiriki na wale watakao shiriki mashindano ya ulimbwende mjini Iringa kufanya usafi katika hospitali ya Rufaa ya Iringa. Zoezi hilo lilianza saa 2 asubuhi hadi saa 4. 

Mwandaaji wa ulimbwende Iringa Miss Maya alisema wameamua kuhakikisha Iringa inakuwa safi na watafanya usafi kila mara mpaka mji ung'are. 

Naye Meya wa Manispaa ya Iringa, Mh. Kimbe aliwaomba wadau wote wajitokee kufanya usafi kwa nguvu zote. Mkuu wa wilaya alisema zoezi hili endelevu na wataendelea kuhimiza usafi kwa nguvu zote . Pia alimuomba mstahiki meya kutunga sheria ndogo ndogo kali zenye faini kubwa kwa wanao kaidi suala la usafi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...