Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa PPF  Bw. William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Bw.  Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya   MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.

Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo

Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.
Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara. 

Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C (EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB. 

Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha Jumamosi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...