Scaveter ikisafisha sehemu ya barabara kuanzia Mwenge hadi Morocco kwaajili ya upanuzi wa barabara mbili zinazojengwa kwa fedha ambazo zilitakiwa kutumika katika kusherekea sherehe za uhuru ambazo hufanyika kila mwaka Disemba 9 ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli, kazi hiyo imeanza kutekelezwa leo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakigombania bango ambalo limevunjwa katika upanuzi wa barabara kuanzia Mwenge hadi Morocco leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. The mdudu ,msaada tutani ndugu zangu maana nasikia njia zitakua 5 pamoja na hizo za sasa sasa swali langu ni itakua vipi njia 5 maana 5 haigawanyiki au 6 wamekosea kusema?

    ReplyDelete
  2. Aliyekwambia kwamba njia lazima ziwe namba shufwa na siyo witiri ni nani? zikiwa njia 5 poa, asubuhi njia tatu zinapeleka magari town, jioni zinawarudisha wadau makwao, simple.

    ReplyDelete
  3. Njia 5 itakuwa zinatumika 3kwenda mjini 2 kutoka mjini asubuhi halafu 3kutoka mjini jioni na 2 kurudi mjini jioni na pia njia ya katikati ndo itakuwa inabadilisha matumizi kwa asubuhi na jioni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...