Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.

Amesema kuwa Benki kuu ilifanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma,malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walishindwa kuvumilia kwa hiyo tetesi tukazipata, wakaguzi wa benki kuu walifuatilia malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki, ambapo fedha kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa kwenye kampuni ya Kampuni ya Egmwa na siku chache zilitolewa zote kwa fedha taslimu wala benki haikukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa. 
TAARIFA KAMILI SOMA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ama kweli nchi ilioza..., yaani kila sehemu ilikua ni wizi tu!!.. Kweli Allah ndie mlipaji kwa yote. Ina maana Kama kulikua hakuna uongozi bali genge' la watu flan lilikua kwenye biashara ya unyonyi' tu

    ReplyDelete
  2. Hii mbaya sana watu hawana uchungu na nchi, wanatunisha matumbo yao, sasa wataona cha mtema kuni, HAPA KAZI TU, Longlive Magufuli, nakumuka mwimbo wa zamani " Mabepari walia, mabepari walia kutaktiwa mirija...".Na hii ndo mwanzo tu, kama sinema basi ni "trela" hii, sinema bado haijaanza. Mafisadi wakome na kukoma.

    ReplyDelete
  3. "................matata, hiya!"

    ReplyDelete
  4. Hivi miiko ya uongozi iko wapi. Mfanyakazi anafungua kampuni ambayo itafanya kazi ya idara ya mfanyakazi huyo serikalini. vipi haki itatendeka kwa makampuni ya uwakala au ukandarasi? tatizo la mgongano wa maslahi (conflict of interest).

    Itapidi JPM turudie azimio la arusha, lililenga uadilifu. kuepuka mgongano wa maslahi (conflict of interest).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...