Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani  amefafanua jinsi mabavyo Tume ya taifa ya uchaguzi ilivyo gawanya vituo vya wapiga kura kote nchini. Katika ufafanuzi huo amefafanua mambo makuu Mawili.

1. Namna ambayo siyo sahihi ya kuhesabu vituo vya wapiga KURA kama walivyo fafamua baadhi ya watu, Ambayo ni namna ya KUPOTOSHA NA NI UWONGO, na

2. Namna SAHIHI  ya kuhesabu vituo kama tume ye taifa ya uchaguzi ilivyo hesabu. Nia hii inazingatia mambo yafuatayo.
i). KUTUO HAKITAZIDI WATU 450
ii). KITUO KINAWEZA KUWA NA IDADI CHINI YA WATU 450
ILI WATU WALIOJIANDIKISHA KITUO KIMOJA WASIHAMISHWE KWENDA KUJAZIA ENEO JINGINE.

Itakuwa hivi.
Endapo kuna eneo ambalo watu waliojiandikisha ni 1900 Tume ya taifa ya uchaguzi itagawanya watu kama ifuatavyo:-
450+450+450 = 1300
1900-1300 = 550
550 gawanya kwa 2 = 275

KWA HIYO MAHALI PENYE WAPIGA KURA 1900
PATAKUWA NA VITUO VITANO (5)

1. KITUO CHA KWANZA WATU 450
2. KITUO CHA PILI WATU           450
3. KITUO CHA TATU WATU        450
4. KITUO CHA NNE WATU          275
5. KITUO CHA TANO WATU       275
JUMLA                                            1900

ZINGATIA
Kutokana na kuwepo kwa vituo vyenye idadi ya watu chini ya 450 kumefanya idadi ya vituo iwe kubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Rekebisha maandishi iwe hivi

    450+450+450=1350
    pia

    1900-1350=550

    Asante.

    David-Kurasini

    ReplyDelete
  2. Huyu mtu wa NEC, asitufanya sisi hatujui hesabu.
    simple arthematic;
    kama ameandisha watu 23,700,000
    vituo vya kupigia kura; 72,000
    Anatakiwa tu kuchukua

    Watu 23,700,000 kugawa kwa Vituo 72,000 ni sawa na watu 329.1666666667
    kwa kukaribisha namba ya karibu hiyo Sawa na watu 330 kwa kila kituo.
    YEYE HIYO 450 AMEITOA WAPI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...