Hii ni kufuatia mkutano mkubwa wa Injili unaoendelea jijini Pretoria (Encounter Conference 2015) ulioandaliwa na Huduma ECG inayoongozwa na Major Prophet Shepherd Bushiri na kurushwa LIVE na Prophetic Channel. 
Wanaohudumu katika mkutano huu ni Major Prophet Eubert Angel, Major Prophet Shepherd Bushiri na Dr. Ramson Mumba na miongoni mwa washiriki WAKUU wa mkutano ni Pastor Sayo Mwanyongo wa kanisa la ECG Dar es Salaam. 
Baada ya mkutano huu kuisha Pastor Sayo Mwanyongo kwa kibali alichopewa na Baba yake Major Prophet Shepherd Bushiri amewaandalia wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani Mkutano mkubwa wa Injili utakofanyika katika viwanja vya kanisa la ECG Dar es Salaam, lililopo Makongo Juu karibu na Chuo Kikuu cha Ardhi kuanzia Ijumaa tarehe 4 hadi Jumapili tarehe 6 kuanzia saa nane mchana. 
Mada ya mkutano huu ni Chukua Miujiza ya Kushangaza kwa Nguvu!. Katika mkutano huo watu wote wataombewa wakiwemo wagonjwa na wote waliofungwa na nguvu za giza na kupakwa mafuta ya Lion of Judah yaliyoandaliwa na Major Prophet Shepherd Bushiri. 
Pia siku ya Jumapili washiriki wote wa mkutano watapata fursa ya kushiriki chakula cha Bwana.
Huu sio mkutano wa kukosa! 
Watu wote mnakaribishwa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...