Na MatukiodaimaBlog
CHAMA
Cha mapinduzi ( CCM)
mkoa wa Iringa kimefuta matokeo ya kata tatu za jimbo la
Kilolo matokeo yaliyokuwa yakimpa ushindi mkubwa mbunge anaemaliza muda
wake Prof
Peter Msola na kuagiza uchaguzi huo kurudiwa kesho
Matokeo
hayo ambayo yamekataliwa na wagombea wote yanadaiwa kupachikwa katika
vituo vya kata hizo tatu japo hata hivyo hayana uhalisia ukilinganisha
na idadi ya wanachama wa maeneo husika .
Katibu
wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga alisema kuwa kutokana na
dosari mbali mbali ambazo zilijitokeza katika kata hiyo ambazo ni
Nyalumbu , Lugalo na Uhambingeto alisema kilichoonyeshwa ni matokeo
hayo kuwa tofauti na matokeo halisi ambayo mawakala wa wagombea
walikuwa nayo na katika kata hiyo makatibu matawi na kata wa CCM
hahakuweza kupeleka matokeo kwa wakati kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi
hadi alipoyafuata na kuona kasoro hiyo .
Katibu
huyo alisema karatasi zilizoonyesha ushindi wa mgombea mmoja Prof
Msolla zilikuwa ni tofauti na karatasi halisi zilizotolewa na chama
hivyo kutokana na utofauti huo wagombea wengine waliweza kugomea
matokeo hayo .
Aibu.......ahahhahahah ndio magori ya mkono hayo ndani ya chama???+
ReplyDelete