Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya kumbukumbu na Habari John Haule, Afisa habari Mwandamizi wa baraza la Taifa la Ujenzi, Robertha Makinda, Afisa Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Dr. Leonard Chamuliho akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na majukumu na mafanikio ya araza la Taifa la Ujenzi. kutoka kulia ni Afisa habari wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Shukuru Sekondo na Mkuu wa Idara ya Majengo, Julius Mamiro.
Afisa Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Dr. Leonard Chamuliho akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Afisa habari Mwandamizi wa baraza la Taifa la Ujenzi, Robertha akionyesha kitabu cha mkataba wa baraza la taifa la Ujenzi.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Dr. Leonard Chamuliho wakati akizuingumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Zaidi ya migogoro 153 inayohusu masuala ya ujenzi imetatuliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi katika kipindi cha miaka kumi kuanzia 2005 hadi 2015.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la ujenzi Dkt. Leonard Chamuliho amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akieleza mafanikio ya Baraza hilo mbele ya waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, tangu mwaka 1982 baraza limekuwa likijihusisha na usuluhishi wa migogoro ya ujenzi nchini na pia lina orodha ya wasuluhishi ambao husajiliwa kutokana na sifa zao ambazo huweza kutumiwa na wateja.

“Utatuzi wa wa migogoro ya ujenzi umehusisha sekta mbalimbali zikiwemo za kiserikali, mashirika ya maendeleo ya nje na ndani ya nchi, taasisi za uendelezaji na usimamizi wa vyama vya kitaaluma, wakandarasi, na sekta binafsi,”amesema Dkt. Chamuliho.

Baraza la Taifa la ujenzi ndilo kitovu cha uratibu kwa taasisi zinazoshughulika na masuala ya ujenzi ili kuleta umoja, uwiano na ushirikiano katika utendaji ndani ya sekta ya ujenzi.

Aidha, Dkt Chamuliho amebainisha baadhi ya majukumu ya Baraza hilo kuwa ni kuhamasisha na kutoa uongozi wa kimkakati kukuza na kuendeleza sekta ya ujenzi nchini kwa kuzingatia ukuzaji wa uwezo wa ndani ya nchi ili kwenda sambamba na maendeleo ya ushindani wa kimataifa.

Baraza pia hutoa huduma mbalimbali zikiwemo uratibu wa sekta, ushauri,  mafunzo, ukaguzi wa kiufundi, utafiti, uchapishaji na usambazaji wa taarifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...