Muonekano wa Samani za Ofisi ambazo hutengenezwa kwa Ustadi mkubwa katika Viwanda mbalimbali vinavyoendeshwa na Jeshi la Magereza zikiwa tayari zimekamilika kwa matumizi ya kiofisi 


Na Lucas Mboje wa 

Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Utengenezaji bidhaa za Samani kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam Maarufu "SABASABA" kwa Mwaka huu 2015.
Akizungumzia ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amesema kuwa anajivunia ushindi huo kwani kulikuwa na ushindani mkubwa wa Makampuni mengi yanayoshiriki katika Maonesho haya ya Kibiashara yanayoendelea.

"Nachukua fursa hii kwa dhati kuwapongeza sana Maafisa wote washiriki katika Banda letu la Jeshi la Maonesho kwa kazi nzuri iliyowezesha ushindi huo wa kwanza kwa upande wa Utengenezaji wa Samani Bora", alisema Jenerali Minja.

Aidha, Jenerali Minja amewaomba Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam watembelee Banda la Jeshi la Magereza ili waweze kujipatia bidhaa bora pia kuona na kujifunza namna bora ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wao Maofisa wa Jeshi la Magereza wanaoshiriki katika Maonesho haya wameushukru Uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu hususani kufanikisha maandalizi yote muhimu ya kushiriki katika Maonesho haya ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Magereza Tanzania limepiga hatua kubwa ya Maboresho juu ya utengenezaji wa bidhaa bora za Samani hivyo kupelekea kuibuka mara kwa mara Mshindi wa kwanza katika Maonesho mbalimbali ya Kibiashara hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...