Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka anatoa salamu zake za muungano kwa watanzania wote na hasa wanaoishi nje ya Tanzania kwa kuwataka watumie fursa hiyo kuimarisha utanzania wao na kuboresha maisha ya watanzania wote hasa katika Nyanja za kisiasa na kiuchumi tunapoelekea katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Katika salamu zake Mhe. Zoka amewataka watanzania wote waishio nje ya nchi kuyasoma mapendekezo ya katiba mpya kiufasaha na kwamba katika katiba hiyo wao wamepewa hadhi maalum. Ili kufanikisha utoaji wa elimu huo unafanikiwa basi Mhe. Zoka amejitolea kutoa nakala chache za katiba hiyo pendekezwa ambayo ipo katika ofisi za ubalozi mjini Ottawa kwa kila atakayetaka kupitia na kuelimisha wengine, lengo likiwa ni kuelewa kilichomo katika katiba hiyo ambayo imetayarishwa kwa kuzingatia mahitaji ya watanzania wote bila kujali mahali waliko. Aidha amewakumbusha kuwa katiba hiyo inapatikana katika tovuti ya Serikali. 

Katika maswala ya kiuchumi watanzania walio nje ya nchi wameaswa kutumia fursa hiyo nzuri kujitambulisha rasmi katika balozi  mbalimbali za Tanzania na kujiandikisha rasmi ili kuwekwa katika kumbukumbu za nchi hatua ambayo itaisaidia nchi kufanya makisio ya karibu ya pato la nje na kupanga malengo na mikakati ya kukuza uchumi wa nchi. 

Aidha kujiandikisha kutawasaidia kupata huduma muhimu za haraka pale watakapohitaji ama wakati wa dharura ikitokea nchi A imeshindwa kutoa huduma hitajika, “Tukubali kuwa Ubalozi ndio kimbilio la Mtanzania mambo yanapoharibika huku nje. Nyumbani kwa Balozi au katika Ofisi za Ubalozi tuna haki ya kuomba ulinzi toka kwa wenyeji Kama ni lazima kufanya hivyo. Naomba Watanzania muuone Ubalozi na makazi ya Balozi Kama nyumbani kwenu kwani vyote ni Mali ya Jasho la wananchi wa Tanzania”. 
Sehemu ya Watanzania Waishio nchini Canada wakiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Jack Zoka wakati wa Sherehe za Muundano.
Ametoa mfano wa raia 26 wa Tanzania waliokuwa wamekumbwa na ghasia za kibaguzi Xenophobia huko Durban SA ambao jana Serikali ya Tanzania iliwarudisha nchini. Hatahivyo amesisitiza kuwa ni hiari ya mtu kuamua kujiandikisha au kutojiandikisha katika ubalozi wake. 

Kama vile utoaji elimu hautoshi, Balozi wa Tanzania Ottawa Mhe. Jack Zoka amekosoa kwamba bado hatua za makusudi zinahitaji kuboresha jumuiya za watanzania wanaoishi nje ya nchi ili zikidhi haja za watanzania wote kwa kushirikiana na balozi husika ili kwa pamoja kuelekeza nguvu za mapambano dhini ya maadui wakuu watatu wa nchi yetu tukufu ya Tanzania ambao ni umasikini, Ujinga na Maradhi.  

Kwa upande wao, watanzania walioweza kuhudhuria sherehe hizo za Muungano zilizofanyika nyumbani kwa Balozi wao wamekili kuwa kwa kasi ya Balozi Zoka mambo yatakuwa mazuri na wameahidi kujipanga upya, kutafuta viongozi wapya ili kuendana na kasi hiyo.

Mheshimiwa Balozi anaandaa utaratibu utakaomuwezesha kukutana ana kwa ana na jumuiya zote za watanzania hapa Canada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...