Na Bashir Yakub.
Kifungu cha 18 cha Sheria ya Kanuni za adhabu sura ya 16 kimeeleza hatua ya mtu kujikinga mwenyewe, kumkinga mwenzake , mali yake mwenyewe na mali ya mwenzake. Kujikinga( defence) maana yake ni kujilinda au kujitetea inapokwa imekutokea dharula ya kuvamiwa na mtu au watu waovu. Uovu ni uovu si lazima awe mwizi . Hata mtu asiyekuwa mwizi lakini amekuvamia kwa nia ovu iwe nyumbani, kazini au sehemu nyingine yoyote basi ni adui unayepaswa kujikinga naye.
1.KUJIKINGA NI HAKI YA KILA MTU.
Haki ya kujikinga na adui si tu imeelezwa katika kifungu nilichotaja bali pia ni haki ya msingi ya kikatiba. Haki hii pia huingia katika zile haki ambazo huitwa haki za kuzaliwa ( in born right). Haki za kuzaliwa ni zile haki ambazo sio lazima ziwe zimeandikwa katika sheria fulani halafu ndipo mtu azitekeleze . Ni haki ambazo hata kama hazikuandikwa popote mtu ni lazima azipate tu. Kwa mfano haki ya kula au ya kuishi.
Haihitaji iwe imeandikwa popote katika katiba au penginepo ili uweze kula au kuishi. Ni kitu ambacho hutokea moja kwa moja( automatic). Ni kitu ambacho huandikwa kama haki katika sheria lakini hata kisingeandikwa ilikuwa ni lazima kiwepo. Halikadhalika ndivyo ilivyo katika haki ya kujikinga ( defence) kwani haihitaji kuwa imeandikwa popote kuwa mtu akikuvamia kukudhuru ujikinge naye. Inakuja tu moja kwa moja mtu akitaka kukudhuru ni lazima ujilinde kwa kutafuta namna ya kujiepusha naye.
2. INARUHUSIWA KUJIKINGA HADI KUUA.
Kifungu cha 18c cha sheria hiyohiyo ya kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu anaweza kujikinga mwenyewe, mali yake , kumkinga mtu mwingine, mali ya mtu mwingine dhidi ya hatari au shambulio mpaka kufikia hatua ya kuua au kusababaisha madhara makubwa ya kimwili. Madhara makubwa ya kimwili ni pamoja na kukata kiungo cha mtu mfano mguu, mkono, au kusababnisha madhara mengine kama kusababisha kidonda kikubwa na hali nyingine zote zinazofanana na hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...