Dkt.
Amosy Ephreim M'Koma, Mtanzania, Bingwa katika fani ya Upasuaji (Colon and
Rectal Surgery). ametambuliwa na Jarida kubwa la watalaam mabingwa wa upasuaji
duniani la "World Journal of Surgical Procedures" kutokana na
shughuli zake za utafiti (Surgical Sciences) katika Chuo Kikuu cha Vanderbilt University huko
North Nashville, Tenesee. Dkt. M'Koma amekuwa taarifa kuu katik
toleo la sasa la Jarida hilo (BOFYA HAPA) lenye bodi ya wahariri 275 ambao wote
ni mabingwa wa upasuaji toka sehemu mbali mbali dunia. Globu ya Jamii
inampa hongera sana Dkt M'Koma kwa fanaka hiyo ambayo kupatikana kwake ni
lazima uwe jembe kweli kweli kwenye fani hiyo.
Kumjua zaidi daktari pingwa
Hongera sana Dkt M'Koma.
ReplyDeleteMichuzi safi kuwaweka wataalamu angalau balance iwepo, tunaona wasanii wamezidi sana kuwekwa, hongera sana profesa kwa kupeperusha bendera ya tanzania.
ReplyDeleteHongera baba, lkn ingekuwa raha angekuwa anafanyia kazi zake hapa hapa tz
ReplyDeleteHongera sana kwa nafasi hiyo. Leteni maendeleo nyumbani sasa jamani kwa elimu mulizopata huko nje. Leteni vifaa vya kisasa nyumbani na tujenge nasi hospitali bora tuache kwenda India na S.A. Tanzania tukiamua tunaweza kabisa
ReplyDeleteLoh! eti alete maendeleo nyumbani wapi Tanzania? Hell noooo! BIIg NO! unamkumbuka Dr. MAssawe wa Hospital ya Moyo? unamkumbuka Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar? na Unamkumbuka Dr. Muhongo? waje Nyumbani halafu yawatokee hayo? kama ningekuwa namjua ningemwambia akae huko huko!
ReplyDeleteHongera Daktari tunakutakia mema unapoendelea kuchangia katika fani hii nchini na nje ya nchi. Endeleza kazi nzuri ikiwemo ya kupeperusha bendera ya wataalamu wa kitanzania..
ReplyDeleteIko poa
ReplyDelete