Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall  Bwawani Mjini Zanzibar.
 Mwanamitindo marufu wa Zanzibar Farouk Abdillahi akimkabidhi Tunzo ya Video bora mwaka ya Taraab Bi. Saada Nassor
 Meneja wa Zenji Entertainment Seif Moh'd (kushoto) akimkabidhi tunzo Mwanamuziki Bora wa kiume wa tarabu asili Cholo Ganun
 
 Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora)  Dkt. Mwinyihaji Makame akimkabidhi tunzo ya muandaaji bora wa Tamasha Zanzibar Music Award mwaka 2015 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa Redio ya Zenji FM Mohamed Seif Khatib katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Mjini Zanzibar. 
 Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Dkt. Mwinyihaji Makame katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Zanzibar Midia Corporation LTD. Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar. Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...