Hayati John Komba enzi za uhai wake
Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kepteni John Komba amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam, mtoto wa Marehemu Bw. Herman Komba amethibitisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. 'KOMBA' TUTAKULILIA (R.I.P.)

    Poleni sana poleni, ndugu yote familia,
    Rafiki nje na ndani, na kuzunguka dunia,
    Ndio kazi ya 'Manani', tuwe pole Tanzania,
    Yarabi mlaze pema, 'Komba' tutakulilia.

    Nnashindwa kuamini, khisi kama mwatania,
    Hatunae duniani, 'John Komba' tukimbia,
    Pengo ataziba nani, sifaze alotimia?
    Yarabi mlaze pema, 'Komba' tutakulilia.

    Kweli hatunae 'Komba', kesheiaga dunia?!
    'Mashallah' kwa kuimba,katu wa kumfikia,
    Jukwaani akitamba, hilo wengi tutalia,
    Yarabi mlaze pema, 'Komba' tutakulilia.

    Alimwimbia 'Mwalimu', nchi nzima jinamia,
    Katika zote awamu, nyimboze zilichangia,
    Masikini yake 'zamu', nani atamughania?
    Yarabi mlaze pema, 'Komba' tutakulilia.

    Nazidi lizwa na mengi, mema yake kiwazia.
    Khasa nyimbo zake nyingi, ndipo wengi mjulia,
    Alo kipenzi cha wengi, 'Mola' mwita itikia,
    Yarabi mlaze pema, 'Komba'tutakulilia.

    Mwenyeez Mungu mlaze pema peponi aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya CCM Kapteni John Komba - AMEN.






    ReplyDelete
  2. R.I.P. Komba utakumbukwa daima kwa nyimbo zako na kikundi chako cha Baby Tot. Pumzika kwa amani.

    ReplyDelete
  3. R.I.P captain

    ReplyDelete
  4. Oooh God !!!! Michuzi Marehemu aliugua? Mbona hatuna taarifa jamani ,bwana awape nguvu ndg wa marehemu!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu hakueka sheria au kanuni kuwa ili ufe lazma uumwe.muda wako ukifika unaondoka tu,iwe kwa sababu au bila ya sababu.

      Delete
  5. R.I.P Captain.
    Utakumbukwa kwa nyimbo zako na sauti nzuri

    ReplyDelete
  6. Overweight,sugar ,bp lets try to be fit overweight aint a good thing

    ReplyDelete
  7. Nimesikitika sana kusikia habari ya kifo chake. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

    ReplyDelete
  8. Nyimbo nzuri za TOT chini ya uongozi wa Bwana Komba zikituhamasisha toka enzi za mwalimu Nyerere tutazikumbuka. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...