Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Vuai Ali Vuai wakielekea kushiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.


Kinana amemaliza ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar ambapo amekagua na kushiriki ujenzi katika miradi 40 mikoa 12. 

Katika ziara hiyo,Ndugu Kinana alijionea mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, zikiwemo barabara, hospitali, elimu na maji pamoja na kusambazwa umeme karibu kila kona. 

Katika ziara hiyo ,Ndugu Kinana amewataka viongozi wa dini na Serikali kukemea kitendo cha CUF kuwaita wanaohamia CCM makafiri. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimpongeza Ndugu Kinana kwa ziara yake, kwamba imekuwa ya mafanikio makubwa na imewapa somo na moyo wa kuimarisha chama visiwani.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji Migomba katika shamba la Ushirika  la Utandawazi Cooperative Society katika kijiji cha Chokocho,jimbo la Mkanyageni,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na mmoja wa viongozi wa Ushirika huo alieleza mbele ya Kinana kuwa Ushirika huo una jumla ya watu 25,na wanajishughulisha na ufugaji wa Kuku wa Kienyeji,Mboga mboga pamoja na Migomba katika shamba lenye ekari mbili na nusu.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kushiriki upandaji wa Mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15.

Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM<ndgu Kinana alipokuwa akiwahutubia leo katika uwanja wa mpira wa Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Ndugu Kinana amehitimisha ziara yake ya siku 15 ndani ya Kisiwa cha Pemba  jioni ya leo,Kuhimiza na kukagua uhai wa chama cha CCM.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza mbele ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa mpira wa Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.Ndugu Kinana amehitimisha ziara yake ya siku 15 ndani ya Kisiwa cha Unguja na Pemba  jioni ya leo, ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

PICHA NA MICHUZI JR-WILAYA YA MKOANI KUSINI PEMBA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kweli huyu katibu anafaa sana, huenda hana hadhi ya kugombea Urais, by the way anafaa sana kuwa kiongozi shupavu.

    ReplyDelete
  2. Naona Katibu Mkuu CCM haihitaji nusu mkeka wala kapeti wakati akishirikia latika shughuli za upandaji miti, mboga wala kuweka jiwe la msingi, maana viongozi wengine wanaogopa sana ardhi ya nchi hii Tanzania.

    ReplyDelete
  3. anamshupalia nani awe shupavu unatakiwa asiwe fisadi na anayelinda mali ya asili ya wala hoi.ushupavu wa nini

    ReplyDelete
  4. Hapa Pemba mikutano ya hadhara ya CCM inafanyika bila ya bugudha ya polisi. Wala hakuna tishio la ugaidi kama ilivyotokea Mbagala. Cha ajabu zaidi ni kua hapa Pemba Ndio ngome kuu ya chama cha CUF. Muheshimiwa Kinana amefanya mikutano yake bila kubugudhiwa.Sasa inafaa tujiulize nani hasa anaesababisha vurugu kati ya polisi na upizani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...