Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akiwakaribisha Wanahabari ambao wakitembelea gerezani hapo Desemba 19, 2014. Wanahabari hao wapo katika ziara ya kikazi katika miradi mbalimbali ya Uzalishaji mali inayotekelezwa kwa mafanikio makubwa na Jeshi la Magereza(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mororogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula.
 Wafungwa wa kike wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro wakifuma mashuka katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza hilo. Wafungwa hao wanapitiwa ujuzi wa aina mbalimbali ikiwemo Ushonaji wa nguo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu za Urekebishaji ndani ya Magereza hapa nchini.
 Muonekano wa mashuka na foronya zake yanayofumwa na Wafungwa Wanawake katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro.
 Wanahabari wakionja chakula cha Wafungwa katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014(kulia) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Habari Leo, Bi. Regina Kumba(kushoto) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Daily News, Bw. Finning Simbeye(katikati) ni Mwanahabari kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Bi. Rose Mdami.
 Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akipokea rasmi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Wanahabari hao kwa ajili ya Wafungwa wa kike gerezani hapo walipotembelea Gereza hilo 
 Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akikabidhi msaada huo kwa Mfungwa wa Kike ambaye ndiye Nyampara Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro. Wafungwa wa Gereza hilo wamewashukru Wanahabari hao kuwatembelea pamoja na msaada huo walioutoa na wameahidi kuwa raia wema mara wamalizapo vifungo vyao.

Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira - Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wanahabari walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kato Rugainunula(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...