DSC_0012
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.

Na Mwandishi wetu
MATAIFA manane  yaliyopo katika nchi zinazoendelea zitaanikizwa mafanikio ya Tanzania katika utekelezaji wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) inayosimamiwa na  Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF).
Pamoja na upelekaji wa maarifa yaliyopatikana nchini Tanzania katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo ambao ulianza mwaka 2012 na kumalizikia 2015, Watanzania ndio watakaotumika kupeleka maarifa mapya.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa UNCDF, Peter Malika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha ya siku tatu inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau mbalimbali wanaohusika na programu hiyo.
Wadau hao ni waandaaji wa miradi, watoa fedha na wasimamizi wanaofanya maamuzi.
Alisema baada ya mafanikio ya mradi huo, UNCDF imemua Tanzania kuwa makao makuu ya LFI na kwamba watanzania baada ya kuonesha uwezo wa dhana za LFI, mafanikio hayo katika mataifa mengine.
Mataifa yaliyoelezwa kupelekewa utaalamu wa watanzania kuanzia awamu ya pili inayotarajiwa kuanza mwakani hadi mwaka 2017 ni Uganda, Benin, Senegal na Bangladesh.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...