Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii

MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo imetupilia mbali maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma, iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa kuwa wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.

Kadhalika, mahakama hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.

Uamuzi huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Mh. Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.
Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria.
Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.
Awali,  Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa maombi yake ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.

Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.

Mapema mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha maombi ya pingamizi la awali ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.

Katika kesi ya msingi iliyopewa usajili  namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.

Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wengi tulitegemea hili. Kimsingi, Kubenea hakuwa na nia ya kusitisha bunge bali kutafuta umaarufu uchwara. Ameshindwa kufungulia gazeti lake ataweza kusitisha bunge? Kwanini Kubenea anapoteza muda wake wakati hata elimu yenyewe ya uandishi hana badala ya kwenda shule angalau akasoma na kuacha kuandikiwa makala na watu wengine yeye akapachika jina?

    ReplyDelete
  2. Michuzi nadhani sasa uangalie uwezekano wa kuweka kidude cha like, natamani nimgongee like anony wa kwanza ila hapa nashindwa

    ReplyDelete
  3. Hao waliosoma wanafaida gani katika nchi hii adhimu ya Tanzania iliyojaa kila aina ya mali inayopatikana hapa Duniani!

    Hacha dharau na kejeli, kubwa zima linatoa maneno ya fedhea! Ulilazimishwa kutoa maoni? Kama huna cha kuchangia kaa kimya, siyo unakashifu watu!

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa kwanza na wa pili, watu kama nyie ndiyo hamjui hata haki zenu, Kubenea katumia haki yake ya kikatiba, nchi hii ingekuwa na watu wengi wa aina ya Kubenea badala ya majuha bendera fuata upepo kama nyinyi, rasilimali zisingeibiwa na wachache. Mnafurahia pesa za walipa kodi kufujwa na bunge la katiba ya ccm wakati watoto wetu wanasomea chini ya miti wakikalia mawe, barabara ziko kama mahandaki na hospitali hazina dawa. au na nyie ni majizi mnaofaidika?

    ReplyDelete
  5. Aliyetoa comment ya kwanza inaonekana naye mwizi,,hana uchungu na pesa za walipa kodi zianvyotafunwa. Ujinga wetu ndio mtaji wa watawala --badilika kifikra.... hapo baadae watoto zako au wajukuu watakuuliza ulifanya nini ulipoona wizi wa mchana unaofanywa na watawala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...