Ile ahadi ya Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli ya kununua kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo imetimia. 
Taarifa za uhakikia tulizozipata hivi punde ni kuwa kivuko hicho (Mv Dar es Salaam) kilichokuwa kinajengwa huko Denmark leo kimeshuka majini na tayari kuanza safari ya kuja Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kufika/kutua Dar es Salaam kati ya wiki tatu mpaka nne zijazo. 
 Kivuko cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini. 
 Kivuko hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga barabara za New Bagamoyo (Kawawa JCT - Tegeta); ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure - BRT) ikiwemo kuanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili ; ujenzi wa ‘Flyover’ ya TAZARA na UBUNGO ; barabara za pete (DSM Outer Ring Roads); barabara ya Dar es Salaam – Chalinze Expressway; kupanua barabara ya lami sehemu ya Gerezani (KAMATA – Bendera Tatu) kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne; kujenga daraja la Kigamboni linalounganisha Kurasini na Kigamboni, daraja hili linatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa sita. 
 PICHANI CHINI: Taswira mbalimbali zikionyesha Kivuko cha MV.Dar es Salaam kikiwa kimeshushwa majini leo tayari kwa kuanza safari ya kuja Tanzania kutokea nchini Denmark.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hongera na shukrani nyingi Mhe. Rais Kiikwete. Watakukumbuka sana.

    ReplyDelete
  2. Nashukuru Michuzi kwa Breaking News! Lakini mbona ni kama Boti tu hii. Kwani vivuko huvusha watu mizigo na magari, je hiki mbona kama hakina sehemu ya kuingiza magari ama watakuwa wanayabeba kwa Winchi?!!!!

    Nauliza tu nipate kujua

    Observer

    ReplyDelete
  3. Kwa kuanzia na kama kweli wamedhamilia wangeanza na viwili kimoja kinaenda kingine ninarudi kama afanyavyo Azam marine kwenda Zanazibar,sera zetu sio endelevu sijui wanokuja 2015 wana mawazo gani,kufanikiwa katika usafir kwanza kabisa utilize economy of scale as much as possible and then be assured of return load.

    Nasikitika kabisa kuwa hadi sasa Train hiyo ya mwakeymbe imeshindwa kabisa kupata return loads pamoja na ICD zilizozagaa kwenye njia yake..
    any way kwa kuanzia siyo mbaya..

    ReplyDelete
  4. Jamani nisaidieni hii picha kweli ni Denmark? au mashariki ya mbali?. Hii quality ya hizi boti ndogo crew boat sio quality ya europe wala boti lenyewe halina quality ya european. Labda kama hii ni boti nyengine tu, lakini kwa boti ambayo imejengwa denmark haiwezekani ikawa hivi. labda kama watu wameenda kujengengesha Denmark ya gerezani wakaokotea vibarua ikajengwa. kwa mwonekano wangu hii sio boti yenyewe na kama ndio yenyewe, basi watu wamechakachua tayari

    ReplyDelete
  5. kaka michuzi napata wasiwasi na hiyo meli pamoja na kivuko maana haina ushawishi kama kweli ni product ya Denmark. na kama ni kweli basi nahoji competence ya wadenish katika teknolojia na hata hayo mazingira hayana ushawishi hata kidogo

    ReplyDelete
  6. wabongo kwa kukosoa mnatisha, mimi nadhani ni mwanzo mzuri, kwa baadae naamini zitakuwepo nyingi zaidi ya hizo, ikumbukwe secta ya usafiri ipo huru kwa wawekezaji wa ndani na nje, hapo government inakuwa kama kichocheo ili wengine waone fursa hiyo. kuna mdau anahoji hadi muonekano wa karakana, c'mon hada ula karakana ni chafu kama bongo tu, msiwe critic kwenye kila kitu, nadhani kwanza tushukuru kwa hatua hiyo mpaka hapo then tutoe ushauri...

    Hayo ni maoni yangu tu..

    ReplyDelete
  7. Siyo boti ni uchakachuaji tu.......

    ReplyDelete
  8. japo sikosoi nia ya kuleta chombo hiki kusaidia watanzania (nauiunga mkono kwa dhati), lakini nahoji uhalisia wa mazingira - ni Denmark au nchi nyingine? kwa mtizamo wa usalama kazini (health and safety) Denmark hawaruhusiwi kuweka watoto eneo la kazi wakiwa hawana hard hart au safety boots, ukiangalia hizi picha kwa karibu utakubaliana na aliyeuliza hapo juu, hii ni Denmark au ni Bangladesh? nadhani ni swali halali, hasa kutokana na historia ya procurement ya miradi mikubwa. hivi dock yard ya mwanza na Dar zinafanana? labda wenzetu mkiangalia picha hamuoni tunavyoona wengine.......

    ReplyDelete
  9. Pamoja na kuwa tunaunga mkono hoja ya kuleta kivuko kaaajili ya kurahisisha usafiri wa raia, nivema watu wakatoa hoja zao hasa pale kunapooneka kuwa maelezo hayalingani na hali halisi.Watanzania tumekuwa wahanga wa kuletewa vilivyo vibovu siku zote kumbuka
    - Ndege zilizo kuwa za ATC, treni & mabehewa, meli etc

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...