Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Joseph Joseph Mkirikiti amezindua mitambo ya mawasiliano (minara) katikaka kijiji cha Muhukulu na kuwataka raia wa Tanzania wa vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale, Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa vyote vya Mkoani Ruvuma na wale wote wanaoishi mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania kuwa Walinzi kwa mitambo ya Airtel inayowekwa kwa ajili ya mawasiliano isiharibiwe na watu wasiopenda maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizindua Minara hiyo ya ya mawasiliano ya Simu iliojengwa katika kata ya Mhukuru Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania.

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti alisema “juhudi zinazofanywa na Serekari kwa kushirikiana na Makapuni ya Simu ikwemo kampuni ya Airtel ni kumpa mwananchi fulsa ya kuwasiliana na watukatika mambo ya kiuchumi,afya,na elimu na mawasiliano ya kijami”

Amesema pia katika kutatua kero mbali mbali za wananchi, pamoja na mawasiliano ndiyo maana baada ya ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania wananchi walipotoa kero zao kwa Rais ufumbuzi umefanywa wakuiomba Airtel kujenga Mnara .

…”sasa ni juu ya Wananchi kuutumia kwa lengo lililo wekwa ili kutowakatisha tamaa wawekezaji aliongeza kwa kusema Mkirikiti! Meneja wa kanda ya kusini wa Airtel kutoka mbeya Straton Afrikan Mushi amewataka wananchi kutumia mtandao wa Airtel hasa huduma za kibenki ili kuepukana na uporaji wa fedha wanaposafili, pia amewaomba kuwa walinzi wa Minara ya Airtel ‘naomba mfahamu huu mtambo hapa ni kwaajili yenu wote hivyo changamkieni huduma zetu nafuu Zaidi hasa ile ya Airtel Money ambayo itaondoa na kupunguza changamoto nyingi za upatikanaji wa huduma za kibenk katika vijiji na miji ya karibu na mkoa wetu huu” aliongeza Straton

Wananchi wa Mkoani Ruvuma wameishukuru serikali kwa kuweza kushirikiana na Kampuni ya Airtel kupata mawasilino ya uhakika huku injinia wa Airtel Saidi Hanga akiwaahidi wananchi kuto katika kwa mawasiliano

Mnara wa Simu wa Kampuni ya Airtel umekuwa mkombozi pekee kwa wananchi wa Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania ambao walikuwa wakisafiri kwa muda mrefu zaidi ya kilometa 40 kutafuta sehemu yenye kushika mawasiliano kwa kupanda kwenye kilele cha mlima, pia wamesema mawasiliano ya nchi jirani ya msumbiji ukiyapata yalikuwa yatoza fedha pande zote mbili bila kujali nani kapiga simu nani amepokea simu.
Mkuu wa wilaya songea Joseph Mkirikiti akikata utepe kuasiria ufunguzi wa mnara wa Airtel uliopo Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania ili kuboresha mawasiliano katika mkoa Ruvuma na jirani, anaeshudia ni meneja wa kanda ya Kusini wa Airtel Bw Straton Mushi (wakwanza kulia) na meneja masoko wa kanda hiyo wa Airtel Bw Jonas Mbaga (kati) mwishoni mwa wiki, mawasiliano hayo yatazaidia vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale, Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa vyote vya Mkoani Ruvuma.
wananci wakisangili mara baada ya Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti kukata utepe kuashiria ufunguzi wa mnara wa Airtel Mkoani Ruvuma mpakani mwa Tanzania na msumbiji kwa lengo la kuboresha mawasiliano mwishoni mwa wiki,wawasiliano haya yatasaidia vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale, Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa vyote vya Mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...