Kinamama wa kundi la ngoma za  utamaduni la Simba kutoka kijiji cha Nhambi, Wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma wakitumbuiza kwa ngoma ya Kigogo huku wakiwa wamekula uzi wa Man U wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa maji uliofanywa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 29, 2014 katika kijiji cha Chunyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. wangevaa uzi wa taifa ningewaelewa, tupende vya kwetu jaman, mngejua wazungu wanavyotudharau wala tusingejipendekeza namna hiyo. Uingereza ni vigumu kuona mtu kavaa uzi wa Madrid ama Barcelona wanapenda vyao.

    ReplyDelete
  2. the mdudu.hivi haya maajabu ya kijinga yametoka wapi? katika hii tanzania yetu mpaka kuvaa hiyo mijezi ya team za nchi za wengine? ni bora wangevalishwa jezi za team yetu ya taifa letu la tz, na ninani hasa aliewaluhusu hao vichwa maji kuvaa hiyo mijezi ya mashetani,, mm naowaombeni sn kwenye hii katiba tuweke vipengele vya kubana ujinga ujinga kama huu coz vyakwetu kwanza vya wengine baadae ikiwezekana malufuku kabisa vya wengine iwe zamu yao kuvaa vyakwetu.

    ReplyDelete
  3. Hii sio ajabu jamani kwani huu mpira wa England umekuwa na mashabiki wengi Duniani nandio maana tuna ziona hizi timu zina zunguka na kuuza Jezi zao sehemu mbalimbali Duniani na nichanzo kikubwa chamapato yao.

    Tunajua kama hizi timu zina mashabiki Asia na semu nyingine nyingi.
    Kwahiyo tuwaache ndugu zetu wafurahi tuu.

    ReplyDelete
  4. Poeni ndugu poeni, naona mnatoka macheche mdomoni bure. This is entertainment, na naona wamependeza sana.Wazungu wote hawatudharau,that is generalisation. Kuna wazungu wanadharau wabantu, kuna wabantu wanadharau wazungu,kuna warabu wadharau wahindi,kuna wachina wadharau wajapani, that is life, if you cant stand the heat get out of the kitchen.Picha hii nimemwonyesha shabiki namba one wa Manu, ambaye siku hizi ni mnyonge kama yuko matangani kwa kuwa timu yake yagaragazwa vibaya, na imemfanya afurahi sana, kuwa Manu watu bado waipenda na hawajaisahau.Wewe ndugu yangu unaesema uengereza ni vigumu kuona mtu kavaa uzi wa Bacellona au Madrid, wataka nikuletee picha za waliovaa uzi wa Germany, Brazil, Spain, Tanzania?Karibu uwe mgeni wangu ujionee mwenyewe mambo na ujifungue macho

    ReplyDelete
  5. Khiyari yashindwa utumwa, walijisemea wahenga maneno hayo. Hao sio kuwa hawakujuwa kuna uzi wa Taifa, la khasha! Pia yawezekana wao wamepewa tu wavae pasina kuzingatia the logic behind. Kadhalika yawezekana pia kukawa kuna mdhamini aliyejitolea kufanya hilo kwa dhamira yake binafsi who knows! Kwa hiyo, tutakapoanza kutowa maoni yetu kwa chuki za upinzani wa kimichezo, tutakuwa tunakosea, mana kila mtu ataanza kuponda, kupongeza au kuropoka kivyake. Uzi wa Taifa upo na naamini walilijuwa hilo, hata Vitenge ya Taifa vipo, wangeamuwa kuvaa pia au hata Kaniki zetu zipo pia wangeliweza kutupia. Uzalendo hata kwenye vitendo pia upo na unaweza kudhihirika na sio kwenye kivazi tu!

    ReplyDelete
  6. Nafikiri inategemea ni jinsi gani unaichambua hii mada. hata hawa watu wanaowakejwri hawa waliovaa hizo jezi
    huenda wala hawaangalii mpira wa timu zetu.
    Wanaangalia mpira wa nje tu.sio wazungu wote wanawachukia waafrica. kuna waafrica pia wanawachukia wazungu pia.we are living in an imperfect world so take heart and be good to others. and not because they hate,then you should hate them as well. Extend your love to others not hate.God bless

    ReplyDelete
  7. Watu kwa kukurupuka! Michuzi kaweka hii baada ya Man U kudroo! Au nyie hamjui michuzi ni mtani wetu huyo toka Liverpool teteteh teteteh :-) :-)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...