Na Dotto Mwaibale

ULAJI wa nyama nyekundu imeelezwa uchangia kwa kiasi kikubwa kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti ambao umekuwa ni tishio duniani.

Hayo yalibainishwa na Daktari  bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti Profesa Anthony Pais kutoka Bangarole India katika semina ya siku moja kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya iliyofanyika Dar es Salaam juzi.

“Ulaji wa nyama nyekundu na vyakula vyenye mafuta unachangia kwa kiasi kikubwa kupata ugonjwa huo ambao umekuwa tishio duniani” alisema Pais.

Profesa Pais alisema mfumo wa maisha wa kula vyakula bila mpangilio na kukosa kufanya mazoezi pia ni moja ya sababu inayoweza kumsabishia mtu kupata ugonjwa huo.

“Ni muhimu kujenga tabia ya kufanya mazoezi walau kwa dakika 20 kila siku itasaidia kupunguza changamoto ya ugonjwa huo.
Akizungumzia ugonjwa wa saratani ya matiti alisema hauwapati wanawake pekee bali na wanaume lakini kutokana na kukuwa kwa teknojia mpya wamekuwa wakiutibu bila ya kuliondoa titi lenye matatizo.

Alisema hivi sasa dunia imekuwa ikitumia gharama kubwa kwa matibabu ya  ugonjwa wa saratani huku vikifunguliwa vituo vingi vya kutibu ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela alisema ni muhimu sasa kwa madaktari wa kitanzania kujifunza teknolojia hiyo ya upasuaji wa saratani ya matiti bila ya kuliondoa titi husika.

Mshauri  wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira ambaye amemleta Profesa huyo hapa nchini amesema baada ya kuona changamoto ya ugonjwa huo aliona ni vema kumleta mtalaamu huyo ili kuona namna ya kusaidia.

Alisema profesa huyo pamoja na kutoa mafunzo hayo mafupi pia atapata fursa ya kutembelea mikoa kadhaa ya kanda ya kati ili kutoa uzoefu wake kuhusu ugonjwa huo.

Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ilidhamini semina hiyo iliyofanyika Hoteli nya Protea Courtyard kupitia vinywaji vyake vya Windhoek Draught na Windhoek Lager.
Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akizungumza katika semina hiyo. Kampuni hiyo ilidhamini semina hiyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira.
Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hawa madokta nawaheshimu, they do a lot of good. But they have a habit of scaring us:
    Jamaa sema nyama ni hatari,kuna wengine wasema pombe(alcohol) atakupa cirrhos,maziwa, too much fat,Sigara,lung cancer,Sukari,kahawa,chocoleti zote zina madhara. Nasikia hata maji(water intoxication)na simu za viganja ni hatari.Where sould I hide?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Doctors knows a lot about health in general, so we have to listen to them, if we want to live long and good health life.

      Delete
  2. Jamani tule nn tenaaa?

    ReplyDelete
  3. ahaha....we anon wa kwanza unachosema kweli.

    Kuna mtu nilimsikia juzi juzi anasema even too much sex sio nzuri. Kwahiyo in the end tutaambiwa hata kuzaa tusizae ili dunia iishe..

    moderation, moderation moderation.... I guess

    ReplyDelete
  4. Do you know that so many disease are caused by poor diet, red meat is a cause of so many disease like diabetes, high blood pressure, colon cancer and some people are dying especially in the developed countries. , it is very important people to be educated about cancer, is very deadly disease, lack of education will cause so many people to die. I am a registered nurse who works in a cancer floor. By eating more vegetable will save your life, this is really. I understand it is very hard for people to change what they eat. But the truth is so many especially young people are suffering from heart disease, diabetes, cancer, poor blood circulation, heart attacks, suddenly deaths, all these are caused by poor diet. Please just educate yourself. REMEMBER YOU CAN LIVE LONG HEALTHFUL LIFE BY EATING RIGHT, EDUCATE YOURSELF. LOT OF PEOPLE ARE DYING YOUNG.

    ReplyDelete
  5. Kuleni mboga za majani jamani khaa!!
    Kwani mmesahau ?hizo hazikutajwa na madhara yeyote.

    ReplyDelete
  6. Mboga za majani zinafaida nyingi katika miilli yetu, zinazuia magonjwa mengi. Miaka ya nyuma watu wengi walikuwa wanakula Mboga sana, watu walikuwa hawaugui magonjwa ya ajabu kama sikuhizi. Mboga za majani ni muhimu sana.

    ReplyDelete
  7. Watz tuna wataalamu wa ugonjwa huu?Hizo info si tunaweza kugoogle tu si lazima kukaa kitako kupotezeana muda. Cha muhimu tukae tujadili njia za kugundua mapema coz every minute count! Iwepo huduma ya kuelimisha wananchi jinsi ya kufanya self exam,kupia matiti kwa mammogram at least every 2Yrs if no issues. Nawakilisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Prevention is cheap than curing. Let us educate ourselves..self breast examination is every month and mammogram is every year. Breast cancer is one of highly killing disease in woman.

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...