Barua ya Wazi kwa Uongozi wa CCT juu ya Tamko la Mapatano ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 48 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania la tarehe 3 Julai, 2014.


•   Sio la Kiponyaji, linatonesha Madonda
•   Watu wa Mungu hawategemewi Kupotosha, Labda Wamepotoshwa

Na John Nkhundi
 Si kawaida yangu kulumbana na viongozi wa dini kwa sababu ya heshima waliyonayo katika jamii na matumaini ya waumini wao kwao.  
Hata hivyo, leo nimelazimika kuandika baada ya kusoma tamko la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) lililotolewa na Mkutano wa Halmashauri Kuu iliyokutana tarehe 3 Julai, 2014 ambalo maudhui yake ni ya kisiasa na limesheni mambo ya dunia.
Tamko hilo lililopewa jina la "Tamko la Mapatano ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 48 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania wa Julai 2-3, 2014" limenistua kwa mambo makubwa matatu. Mosi, tamko hili limetolewa Julai 3, 2014 lakini likatolewa magazetini tarehe 15 Julai,2014 tena katika gazeti moja tu la Mwananchi. 
Mtiririko huu wa matukio yaani muda wa Tamko lilipotolewa na muda lilipochapishwa kunatia mashaka ikiwa ni jambo la kimkakati au nasibu tu. 
Zaidi, upana huu wa muda kati ya lilipotolewa na kuchapishwa kunaleta pia wasiwasi kuhusu uhalisia wa tamko lenyewe. Maana, kwa kawaida matamko ya aina hii hutolewa mara tu Mkutano unapoisha, tena kwa kusomwa mbele ya waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2014

    Of use ukitaka kuponya kidonda ambacho hakikuhudumiwa vizuri itabidi ufumue kwanza, hivyo kutonesha kabla ya kutibu moja kwa moja! Na hii lugha ya watu wa Mungu sio sahihi kwa anayeelewa, kwa sisi sote watu wa Mungu! na kubainisha mpaka wa nani aongelee siasa na nani asiongelee ni vigumu sana, kwani siasa ni maisha ya watu! Hivyo tuwe wavumilivu kusikia maoni tofauti tofauti, wote tuna haki ya kuijenga hii nyumba ya Tanzania! Hivi kuna "roho" ya Taifa? Naona mtoa hoja unazungusha zungusha maneno kuchanganya anayesoma hoja yako! Tuvumiliane "mfalme" anapoambiwa akavae nguo!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2014

    "...dhaifu na mufilisi"!! Hizi ndizo busara wakati unatoa maoni yako?? Hivi hakuna lugha nyingine ya kiungwana?? Kumbuka maneno yanaweza kukuonesha jinsi ulivyo na uko upande gani! Hapa bado tunajadiliana, hoja zote zina mantiki yake. Kutumia maneno makali ni kuonesha ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa, na ndicho kinacholetaga vurugu kwenye nchi!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2014

    Umefanya vema kuandika na kuweka ufafanuzi kadhaa katika vipengere fulani.

    Ila nashangaa na wewe umetumia lugha ya kuwakshifu viongozi wa dini na kuwashambulia kama wewe ndio malaika unayejua kila kitu.Jua moja kuwa uelewa wako si uelewa wao unachokiona si sahihi wewe wao wanakiona ni sahihi.Labda kama ungekutana nao ana kwa ana wangekufafanulia vizuri kwa yale ambayo hujayaelewa na badala yake umewalaumu kuwa wamepotoka kutoa tamko.Unashambulia sana na kumtetea Rais kama vile hajawahi kufanya makosa katika mchakato mzima na uteuzi wa wajumbe wa tume. Waswahili wanasema "siri ya mtungi aijuaye ni kata"

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2014

    nina uhakika hao viongozi wa dini wangekuwa upande unaotaka wala usingekuja hapa kuandika haya

    ni kama mlivyopotosha ile taarifa ya mwanzo eti UKAWA rudini bungeni bila masharti

    mtu mwelewa ni yule anayekubali kukosolewa pia ... no one is perfect ... na rais amefanya makosa kwenye hilo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2014

    Leo nimefurahi kuona maoni murua yenye kujenga yameachwa ni nadra sana....hakika naungana na wote mliotangulia kutoa maoni.....upeo wenu ktk hili ni mpana sana.....huyu aliyeleta mada hii ....anyway...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2014

    Ila maneno yote waliyotamka viongozi wa dini si yana ukweli? sasa tatizo lipo wapi? Kumbuka nchi hii ni ya wote na likitokea tatizo hata viongozi wa dini wataathirika kwa hiyo ni wajibu wao kukemea matatizo mapema ili kuepusha balaa zaidi huko mbele. Pili mwandikaji umechukua upande mmoja wazi wazi na sio busara mchambuzi ukaegemea upande bila shaka una sababu zako za kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2014

    Mleta mada umejitahidi sana kupingana na viongozi wa dini lakini hata sisi tusiokuwa viongozi wa dini wala wa nchi hii tunaona kwamba viongozi wa dini wameongea ukweli. Mleta mada jitahidi kuepuka hisia zako ndizo zionekane za maana zaidi kuliko za wengine. Tuko wengi tunaoungana na UKAWA hasa tunaojali maslahi ya Tanganyika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...