Na mshurukuru Mungu kwa kunipa afya na uzima mpaka leo na mpaka kufikia hapa tulipofika na kuweza kuona miaka zaidi ya hamsini ya uhuru na miaka hamsini ya Muungano  na mpaka kufikia hatuwa ya kuweza kupata katiba mpaya au mchakato wa kuandika katiba mpya,
Na wewe Bwana michuzi nashukuru kwa kazi yako unayoifanya ya kutupa matukio yanayotokea uko nyumbani kwa video na kwa picha,Mungu akurinde na akupe uzima na Afya.

Bwana michuzi wazungu wanasema  damu ni nzito kuliko maji na kubomoa ni rahishi lakini kujenga ni kazi, nayasema haya sababu Tanzania ya leo inapoelikea kuna njia ambayo ni giza na giza hilo linaweza kuleta janga ambalo lina weza umwagikaji wa damu na tukapata janga ambalo litaifanya nchi kugawanyika na  kuwa sawa sawa somalia kwa udini,ukabila,au South Sudan au nchi zingine zilozoisha pata misukosuko za west Africa liberia, Siera leon nina yasema haya kutokana na kauli zinatolewa  na baadhi ya vyama vya siasa toka vyama vya siasa vilipoanziswa,na maneno ya wabunge wa katiba.

Wa Tanzania miaka hamsini ya uhuru kuna mengi mazuri ambayo yamepatikana na mengine yalishndikana kwa sababu zetu sisi wenyewe au sera za serikari toka tulipo pata uhuru,na katika miaka hii hamsini ya muungano kuna mengi yamefanikiwa na mengine yamechukuwa muda kutatuliwa na mengine yanatakiwa kutatuliwa kwa kuangalia kule tunakotoka na kuangalia nini cha kufanya,

Dunia ya miaka ya 60 ,70,80,90,na leo kunatofauti kubwa sana kwa kifupi wakati nikiwa nasoma miaka ya 80 tulikuwa tupiga simu posta alafu posta ndio inakuunganisha na mtu wa dar au mwanza lakini leo ni sekunde, ndugu wananchi kunamambo mambo ambayo kwa ukweli lazima tuwaenzi wazee wetu hao walio tutangula Mzee Nyerere na Mzee Karume waliamua kujenga nchi mpya nchi yenye usawa nchi ambayo haina makabila nchi ambayo haina dini nchi ambayo ni ya watanzania sio wazungu wala weusi wala wahindi wala waarabu walijenga nchi ya waTanzania ambayo ina lugha moja ni kitu ambacho ni cha kujivunia nchi nying za k iAfrika zinaongea lugha za kingeni lakini Tanzania ina lugha yake ambayo siyo mkoloni.

Ndugu wananchi mimi nimeona vita ya Uganda from 83 mpaka Mzee Museveni alipochukuwa nchi 1986,vita ya Rwanda ya mwaka 1990 mpaka 1994 nimeiona na baadhi ya ndugu zangu walikufa katika hiyo vita na pia nyinyi watanzania mumeyaona na mumeyasikia ya Congo kina dada na kina mama wanavyoeteseka sana wamedakwa na kuuliwa kama wanyama sababu ya kauli za viongozi kuwa na watu wanaotaka madaraka kwa kutumia nguvu au kumwaga damu za wengine na kuwa na watu wanaojiita viongozi kumbe hawana Vision bali ni ma selfish nawaomba muwe macho na viongozi wa vyama vya siasa wawe wa CCM,CHADEMA,CUF,DP,NCCR, yule yoyote anayetumia lugha za kuleta vurugu siogopi  hapa nitasema kabisa Chadema walisema nchi haitatawalika,na juzi hapa katika bunge hili la katiba mwenyekiti wa chama cha CUF Mr lipumba aliwaita wabunge wa CCM eti ITARAHAMWE ni kitendo cha kushangaza kwa mtu aliyesoma mpaka kuwa profesa na kuamua kutumia neno kama hilo katika bunge maana yake Mr lipumba anamaanisha wana CCM wote Tanzania ni ITARAHAMWE nina omba Mr lipumba atupe jibu sababu wabunge wengi katika hilo bunge ni wana CCM

Ningependa kusema Mr Lipumba umesoma na wewe ni mwa siasa na ni kiongozi wa chama omba Radhi kwa WaTanzania kwa kutumia neno ambalo alifai katika bunge la Tanzania na kwa jamii.

Ndugu wananchi nirudi kwenye point ya katiba ni kweli tunataka katiba ya wa Tanzania na siyo ya CCM,CHADEMA,au CUF,NCCR, tunataka katiba ya Jamuhuri ya Muungano katiba yenye usawa katiba ambayo ambayo ina Raisi na makamo wake katiba ambayo ina waziri mkuu wa Tanzania bara,katiba ambayo ina waziri  waziri mkuu wa Tanzania visiwani Zanzibar katiba ambayo inaonyesha madaraka yao katiba ambayo itaongoza Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na katiba inayoonyesha ni nani amri jeshi mkuu  wa Tanzania. ndugu  maoni yangu haya ninayotowakutoka na mambo ambayo nimejifunza katika maisha au tabu namambo ambayo nimeyaona kwenye vita za wenyewe kule Uganda na kule Rwanda.
Ndugu wananchi na ndugu Wabunge, katiba si kitu kidogo na wala si kitu cha kukulupuka mumesema mengi lakini wakati umefika mumetukana lakini wakati umefika mumeitana majina lakini wakati umefika miaka ya hamsini ya uhuru imekuwa na amani na mafanikio  na miaka hamsini ya muuungano pia imekuwa na mafanikio na pia ina mengi amabayo yanatakiwa yafanyiwe marekebisho na ambayo yanatakiwa kufanywa  ninawaomba msifikiri eti kwa vile muko bungeni WaTanzania wengine hawaipendi nchi yao au watakaaa na kuendelea kusikia mambo yasiyo na maana au faida wakati nii huu mkae mutakafari kwa kirefu na muisome katiba kwa kwa kirefu kifungu kwa kifungu alafu mtuandikihe katiba ambayo italeta maendeleo kwa kizazi kinachofata,katiba ambayo ni ya wa Tanzania kama tunaenda kwenye Fedal government muundo ambao utalinda heshima ya nchi na watu wake na kuleta maendeleo.katiba ya ambayo itatujenja kiutendaji kazi katiba inayoonyesha au mwongozo wa uwajibikaji.
Cha mwisho ningependa kuwagusia Amani na maendeleo yaliyoanzishwa na Wazee wetu ndio kitu cha kujivunia kuwatukana au kuwakejeli ni kukosa adabu ni lazima kutumia majina ya kwa heshima na kuelimisha ata kama kuna makosa waliyafanya wao walikuwa ni binadamu kama wewe na mimi.
Bwana michuzi nashukuru kwa  kunipa nafasi hii tena Mungu akubariki

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Mdau Yusef Israel

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Siasa kweli mchezo mchafu.
    Mtu kama Lipumba kubebeshwa ujinga na kina Slaa ni tukio ambalo kwa akili za kawaida huwezi kuliamini. Lakini kwa kuwa ameingia kwenye siasa, basi usomi wake umekuwa, ashakum si matusi, pumba.
    Sasa msomi kama huyu anapobebeshwa boksi la fikra zisizo na akili kama alivoonekana hivi karibuni, najiuliza, nani atabaki.
    Lakini naamini Mwenyezi Mungu bado anaipenda Tanzania yetu na matumaini yangu ni kuwa kama alivyopeperuka Mrema na NCCR yao ya kina Marando, ndivo hivyo hivyo Mwenyezi Mungu atatuondolea balaa la kina Slaa, Lissu na huyu msomi anaeshindwa kuelewa thamani yake, Lipumba.
    Mwenyezi Mungu Mkubwa tuepushe na mahasidi, Amin.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  2. Point well taken.

    ReplyDelete
  3. Ninyi uwaka hamkutumwa na wananchi kwenda bungeni. Bunge la katiba halina wabunge waliochaguliwa na wananchi, sasa mnakwenda kwa wananchi kuwaeleza nini? Bunge la Muungano ndilo lilitumwa na wananchi lakini si hili la katiba. Bakini huko huko bungeni mtoe maoni yenu. Sisi tutapiga kura. Tafadhali sina msitake kutuchanganya. Hamkutumwa na wananchi hata kidogo. Msijipe kazi ambayo hamkupewa na wananchi. Hakuna aliyewachagua kwenda kwenye bunge la katiba. Mimi ninawashangaa sana. Huo uchaguzi wa kuwachagua kwenda kwenye bunge la katiba umefanyika lini. Rudini bungeni mkatimize wajibu wenu wa sheria ya mabadiliko ya katiba. Hatuwataki huku mitaani.

    ReplyDelete
  4. Duh halo umelonga blaza! Uwaka wamechemsha! Rudini mjengoni.

    ReplyDelete
  5. Kashkashi zote hizi ni dalili ya kuwa pande mbalimbali ndani ya Bunge Maalum la Katiba zinatafsiri kazi ya kutunga katiba mpya kwa maono/vision tofauti na kitu hiki ni murua.

    Ni murua maana inakoleza kuleta vikundi kuja na nguvu-za-hoja ambazo zitutumika kushawishi, kuelezea kwa kina uzuri wa hoja na hatimaye MUAFAKA mzuri utafikiwa.

    Kikubwa kazi hii muhimu ya kuunda katiba mpya isiharakishwe kuwa imalizike ndani ya siku 90 bali hoja, vikundi kutoka nje n.k inatupatia nafasi na sisi wananchi na taasisi zingine ambazo hazimo ndani ya mjengo kuchangia na kufuatilia nani kafanya vizuri na nani amepotoka.

    Hii kazi hata ikichukua miaka mitatu (siku miaka tisa) ni sawa tu, kikubwa ni kupata katiba itakayo dumu miaka 200 na kuwekewa viraka vichache huko mbele kwani itakuwa ni KATIBA BORA.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete
  6. Mwasisi wa kudai Tanganyika ni CCM yenyewe.

    Mwaka 1983-4, hapakuwa na Chadema wa CUF bali CCM peke yake kama chama cha siasa Tanzania. Isitoshe, aliyeanzisha vuguvugu la Tanganyika alikuwa na cheo cha Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa - Aboud Jumbe kwa hoja kwamba hati za muungano kuhusu mfumo wa muungano zimechakachuliwa. Je Sultani wa Oman alihusishwa?

    Kundi la Wabunge wa G55 mwaka 1993-4, nao walikuja na hoja ya Tanganyika, na hakuna mbunge hata mmoja aliyekuwa sio wa CCM. Tanzania ilikuwa bado ina chama kimoja, na hapakuwa na Chadema wala CUF. Na rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM taifa (Mzee Mwinyi), makamu wake (john malecela), katibu wakke taifa (marehemu Kolimba), wote waliridhia mchakato wa Tanganyika uanze. Bungeni, makamu mwenyekiti taifa ambae pia alikuwa ni waziri mkuu (malecela) aliridhia uzinduzi wa Tanganyia, huku waziri wa sheria na katiba wa wakati ule (samuel sitta, mbunge wa CCM), akiahidi kuanzisha mchakato wa kura ya maoni. Kwanini hatukusikia Sultani akihusishwa?

    Tume ya nyalali, tume ya jaji kisanga, na nyingine nyingi, ziliongozwa na pia kutawaliwa na wana ccm, na hazikuwa na wapinzani ndani yake, mbona hatukusikia sultani akihusishwa?

    Tume ya katiba chini ya Jaji Warioba, imepita kwa wananchi, na wengi wao wamependekeza serikali tatu, mbona hatukusikia maoni haya yakihusishwa na Sultani?

    Kwa vile CCM ilidhania wingi wao bunge la katiba utawawezesha kuburuza maoni ya wananchi, wale wote walioenda kusimamia upande wa wananchi wanaungana, wanahusishwa na Sultani. Ina maana kusimamia upande wa wananchi kwa mujibu wa rasimu ni kusimamia matakwa ya Sultani?

    CCM imefanya vya kutosha kudharua maoni ya wananchi, na pia kwenda mbali na kuwatishia kwamba maoni na mtazamo wao utapelekea jeshi kuchukua madaraka ya nchi. Sasa kuanza kuhusisha maoni ya wananchi na Sultani ni kuwatusi Watanzania.

    Hata kama Zanzibar itaamua kuwa na mahusiano na Oman, mbona Tanganyika imeuzwa yote kwa mchina?

    Lukuvi ameanzisha jambo la hatari sana kwa ccm na muungano kwa ujumla. Yote yanayoendelea, na mengine makubwa zaidi yatakayofuatia, yatatokana na kitendo alichofanya Lukuvi. Bila ya uongozi wa nchi kuingilia kati, Lukuvi ndio atakuwa ni chanzo cha ccm kufa, muungano kufa, na nchi kuingia katika machafuko.

    Hata waseme serikali tatu kutakaribisha "mwisho wa dunia", Tanganyika haiepukiki.
    CCM izibe sura yake kama inaona aibu, imtengeneze mwana Ccm au wana ccm kadhaa ambao watajifanya kama wana mageuzi ndani ya chama, waje na wazo la kuitaka Tanganyika, na wale walioikataa, wakae kimya. Nje ya hapo, CCM haitapata kura za kuingia Ikulu Tanganyika wala Zanzibar katika uchaguzi utakaofuatia. Wagombea urais ccm Tanganyika na znz watasimama kujinadi vipi? Kwamba watatetea maslahi ya Tanganyia na muungano wa serikali tatu? Mfumo ambao iliukana kwa miaka 50? Wananchi watasema hapana kwani kuwapa ccm wataenda kuhujumu mfumo huo na Tanganyika yake vife.

    ReplyDelete
  7. Hawa ukawa hawana busara tatizo mibuyu mikubwa ndani mbegu chache

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...