Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
 Juhudi ya kulinasua gari hilo zikiendelea kufanyika.
Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa iliponasa kwenye tope.
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo.
 Juhudi za kulinasua gari hilo zikiendelea.
 Eneo linavyoonekana
Gari ikiwa imekwishaondolewa kwenye eneo korofi tayari kwa kuendelea na msafara kutoka Wilaya ya Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,ItIkadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro amemaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Haya basi wakuu, mkirudi Dar msisahau kuwa haya ndio matatizo ya hawa ndugu zetu. Fanyeni maarifa muwatandikie mkeka. waondoleeni hii karaha ya matope.

    ReplyDelete
  2. Nimependa sana mkikutana na hali hizi maana mkikaa mijini huko mnasahau kabisa kama wenzenu ndo tunahangaika namna hiyo kila uchao na hapo magari yenu ya kisasa you can imagine ya kwetu yaliyochoka hali inakuwa vipi its good to feel the pinch may be you will work hard to make things better for all of us

    ReplyDelete
  3. Ohhh hii imekuwa ni sehemu ya Mafunzo kwa Vitendo kwa Makada wa Chama chetu!

    Nadhani CHANGAMOTO HIYO ITASAIDIA SANA MAREKEBISHO YA UTENDAJI WETU KICHAMA ILI AHADI ZA MIUNDO MBINU MAJUKWAANI WAKATI WA UCHAGUZI ZIENDE SAMBAMBA NA MATEKEKELEZO NA KUAKISI HALI BORA KWA WANANCHI HUKO MANYASINI.

    CCM JUUU!!!

    ReplyDelete
  4. Hiyo hali haiko njombe tu, kule kwetu Bunju A- pale bunju shule, Dar es salaam, mvua ikinyesha hali ni kama hiyo kabisaa hamna tofauti tunapata shida sana.

    ReplyDelete
  5. Sehemu nyingine hizi gari linaweza kukuharinbikia halafu hakuna hata mtandao..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...