i

MAREHEMU SUPREME MAESTRO NDALA
KASHEBA
FAMILIA YA ASHURA KASHEBA WA LONDON ,TUNAPENDA KUMKUMBUKA MPENDWA BABA YETU KIPENZI SUPREME MAESTRO NDALA
KASHEBA NI MIAKA 7 LEO TAREHE 22 OCT 2011 ,TOKA AMEAGA DUNIA.

UCHESHI, UPENDO NA UKARIMU WAKO KATU HAUTASAULIKA ,MAWAZO NA USHAURI WAKO UTABAKI MIOYONI MWETU. 

UKO KWENYE MAOMBI YETU KILA SIKU NA TUNAKUMBUKA YOTE ULIYOYAFANYA KATIKA MAISHA UMEBAKI KUWA KUMBUKUMBU KUBWA SANA KWETU JAPOKUWA SIKU ULIPOTUTOKA ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUBWA SANA KWETU. 

HATUUISHI KUKUKUMBUKA NA KUKUOMBEA BABA YETU MPENDWA.

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPA UJASIRI MKUBWA WA KUELEWA KUWA KIPENZI CHETU UMETUTOKA.

SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI,UKAE KATIKA AMANI MPAKA HAPO MWENYEZI MUNGU ATAKAPOTUKUTANISHA TENA INSHALLAH.UNAKUMBUKWA NA
FAMILIA YOTE,WATOTO WAKO WOTE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI TUNAKUOMBEA MAPUMZIKO MEMA. 

MWENYEZI MUNGU AIWEKE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YAKE PAMOJA NA NDUGU WOTE WALIOKWISHA TUTANGULIA MBELE ZA HAKI.

AMIN.

WAKO KIPENZI MWANAO MARIAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...